UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameondoka nchini jioni ya leo,
Jumanne, Januari 24, 2012, kwenda Davos, Uswisi, kuhudhuria mkutano wa mwaka huu
wa Umoja wa Uchumi Duniani
wa World Economic Forum (WEF) unaoanza
kesho, Jumatano, Januari 25.
Katika siku nne za
mkutano huo, mbali na kuhudhuria
mkutano wenyewe ambao hukusanya viongozi wakuu wa siasa, biashara,
uchumi na jamii duniani, Rais Kikwete atakutana
na mlolongo wa watu mbalimbali
kujadili jinsi gani wanavyoweza kushiriki kuwekeza katika uchumi wa
Tanzania.
Shughuli ya kwanza ya Mheshimiwa
Rais Kikwete mara baada ya
kuwasili Davos ni kukutana na Bwana Robert Hormats, Naibu Waziri wa Uchumi,
Nishati na Kilimo wa Marekani,
ili kujadili ajenda ya Afrika
itakayowasilishwa kwenye mkutano wa mwaka
huu wa nchi
tajiri zaidi duniani za G-8 utaoandaliwa na Marekani. Pia viongozi
hao wawili watajadili uhusiano wa kiuchumi
kati ya Tanzania na Marekani.
Baadaye jioni atahudhuria halfa ya faragha
ya ufunguzi wa mkutano wa
WEF mwaka huu itakayoandaliwa na Mwanzilishi wa mikutano hiyo ya
WEF, Profesa Klaus Schwab, na
Alhamisi Rais Kikwete mbali na
kushiriki shughuli za mkutano atakutana
miongoni na viongozi wengine na Rais wa
Benki ya Dunia, Bwana Robert Zoellick; Mwenyekiti wa Bill and Bellinda Foundation, Bwana Bill Gates na
Waziri Mkuu wa Kenya, Bwana Raila Odinga.
Mchana wa siku hiyo, Rais Kikwete
atakuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika vikao
viwili. Katika kikao cha kuzungumzia jinsi ya kuongeza kasi
ya uwekezaji katika kilimo barani
Afrika, Grow Africa Partnership: Accelerating Investment
in Africa Agriculture, Rais Kikwete anatarajiwa kuelezea maendeleo ya Mpango Kabambe
wa Kuendeleza
Kilimo katika Ukanda wa Kusini
mwa Tanzania wa SAGCOT na baadaye atazungumza
katika kikao kitakachojali hali ya baadaye ya
Afrika – Shared Opportunities for Africa’s Future.
Aidha, siku ya Ijumaa,
Rais Kikwete atakuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu kwenye kikao
cha kujadili visheni mpya ya kilimo
ya Afrika – Realising a New Vision for Agriculture: An Action Agenda
na baadaye
atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Australia, Bwana Kevin Ruud na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika
la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID)
Bwana Raj Shah. Pia Rais Kikwete atakutana na Bwana Paul Walsh, mwekezaji katika Kampuni ya Bia
ya Serengeti.
Kwenye siku ya nne na ya
mwisho, miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete atakutana
na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa
Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa
Thailand kabla ya kundoka Davos kwenda Addis Ababa,
Ethiopia ambako atahudhuria
Mkutano wa Wakuu wa Nchi
za Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24
Januari, 2012