UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES
SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Aidha, Rais Kikwete amemteua
Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Hamid Mahmoud Hamid kuwa
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi na Bwana Julius Benedicto
Mallaba kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Desemba 22, 2011 na Katibu Mkuu
Kiongozi, Bwana Phillemon L
Luhanjo mjini Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo
umeanza tokea Jumatatu, Desemba 19, mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi wake, Mheshimiwa Lubuva alikuwa Jaji katika
Mahakama ya Rufani Tanzania na
baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili
ya Viongozi.
Mheshimiwa Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Lewis Makame ambaye mkataba
wake wa utumishi wa umma ulifikia
mwisho Julai, mwaka huu, 2011.
Naye Mheshimiwa Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya
Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi
iliyokuwa inashikiliwa na Mhe Jaji
Omari O. Makungu. Mheshimiwa Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.
Naye Bw. Mallaba, kabla
ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu
ya Mikataba (Contracts and
Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Bw. Mallaba anajaza
nafasi iliyoachwa wazi na
Bwana Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22
Desemba, 2011