DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi mkoani Iringa kuwa
mstari wa
mbele kuwasaidia wananchi kubuni miradi yenye tija
inayoweza kusaidia katika kuongeza kipato.
Rais Kikwete amewambia viongozi hao katika
nyakati tofauti wakati wa kupokea
taarifa za Wilaya Mkoani hapa
ambapo yuko katika ziara ya
kikazi ya kukagua maendeleo na shughuli za
wananchi kwa ujumla.
“Viongozi ndiyo wakuelekeza wananchi kuibua miradi ya
maendeleo na
siyo kuwaachia wananchi, msiache majukumu yenu kwa
wananchi” Amesema.
Rais ametoa maelekezo hayo kwa
viongozi baada ya kuwauliza viongozi
juhudi wanazofanya za kutatua kero
mbalimbali na kusaidia wananchi katika kuboresha maisha yao.
Katika sehemu kadhaa viongozi
wamekuwa wakishindwa kubainisha kwa ufasaha na uwazi
juhudi zao na majukumu ya
kutatua kero ambazo
wananchi wamekuwa wanakumbana nazo na badala yake
kumueleza Rais kuwa matatizo hayo
hayajatatuliwa kwa sababu wananchi hawajaibua miradi.
Rais amewataka viongozi kuwa na mipango
yao wenyewe ya maendeleo pale ambapo wananchi wameshindwa kuibua mipango na fursa
mbalimbali za kimaendeleo kwani hilo ndiyo jukumu
lao kubwa la msingi kama viongozi
na siyo kuwaacha
wananchi wakikabiliwa na matatizo kwa
vile hawajaibua miradi.
“Mkikamia kufanya maendeleo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi mtawasaidia
wananchi kupata maendeleo zaidi, ongezeni bidii ya ubunifu ili
msaidie kuinua maisha ya wananchi”
Ameongeza, “Mnaweza kubadili wilaya na maeneo yenu
kwa kusaidia wananchi kubuni na kuibua miradi
na siyo kusubiri
wao waibue ndiyo muanze kuifanyia
kazi” Amesema .
Rais ametoa mfano katika
nyanja za
kilimo ambapo wafugaji wanaweza kuongeza ubora wa mifugo yao
kwa kutumia njia ya kuhimilisha
(artificial Insemination), kuboresha ufugaji wa kuku wa kienyeji na
hata kwenye shughuli mbalimbali za asili ambazo
wananchi wanazimudu bila kuwa na
utaalamu mkubwa.
Rais amesema ni
jambo bora kama viongozi watakuwa
mstari wa mbele kuhamasisha katika kuibua na
kubuni njia mbalimbali za maendeleo
tofauti na sasa ambapo viongozi
wanasubiri wananchi waibue miradi au mipango yao wenyewe.
Rais amewakumbusha viongozi wa Iringa kuwa
pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli zao za
maendeleo , jukumu kubwa la viongozi ni kuwasaidia wananchi
kwenda mbele zaidi na kamwe
siyo kusubiri mpaka wao waje
na mipango au miradi na kujiuliza
kuwa itakuwaje pale ambapo wananchi hawajaibua au hawana uwezo wa kuibua
miradi yeyote.
Rais amesema ameona wananchi wana jitihada
kubwa mkoani Iringa za kujiletea
maendeleo na
kuridhishwa na juhudi hizo na
hivyo viongozi hawana budi kushirikiana
na kuongeza jitihada hizo katika
mambo yanayoweza kuwaongezea
kipato.
Wananchi katika Wilaya za
Ludewa na
Makete wametoa kilio chao cha kuchelewa kupata mbolea kwa wakati
na umbali wa sehemu za
kununulia mbolea hiyo.
Rais Amesema vitafunguliwa vituo vya kusambazia mbolea katika wilaya za
Ludewa na Makete ili kuwapunguzia
wananchi adha hiyo.
Rais Kikwete anaendelea na ziara ya
Kikazi mkoani Iringa ambapo
pia hutumia mikutano ya hadhara
kupata maendeleo na matatizo ya
wananchi kutoka kwa wenyeviti na
viongozi na kisha kutoa majibu
kupitia kwa wataalamu mbalimbali wakiwemo mawaziri aliofuatana nao, wataalamu wa Wizara
mbalimbali na viongozi wa Mkoa.
Rais ameshatembelea Wilaya za Ludewa, Njombe,
Makete na
leo anatembelea Wilaya ya Mufindi.
Mwisho