DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE amesema anafarijika sana kuona kauli mbinu ya CCM ya mwaka 2005 ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania imetimia. “Leo miaka 5 baadae napata faraja kubwa sana maana tumetimiza ahadi yetu”.  Rais amesema  na kuongeza kuwa ukiangalia yale yaliyofanyika kwa miaka 5 kwa ARI MPYA, KASI MPYA na NGUVU MPYA mambo mengi yamefanyika, Rais amesema hayo leo wilayani Bunda mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuweka mtandao wa mabomba ya umwagiliaji katika Bwawa la Kisangwa lilojengwa na serikali kwa shilingi milioni mia saba na ishirini na tatu na nusu(mil.723.5).

Akifafanua azma ya Maisha Bora kwa kila Mtanzania Rais amesema azma hiyo ina pande mbili ambazo ni mapato ya mwananchi kwa ajili ya mahitaji yake mwenyewe na upande wa pili ni mwananchi kupata huduma za jamii kama vile kupata maji, huduma ya afya, elimu na barabara.  Bwawa la Kisangwa lina ujazo wa mita 750,000 tuta lenye urefu wa mita 8 na upana wa mita 135.

Wilaya ya Bunda sasa ina mabwawa makubwa manne, mawili kwa umwagiliaji na mawili kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo.  Rais ameeleza kuwa jitihada zote hizi za Serikali, ni katika kutimiza mradi wa Maendeleo ya Kilimo na Mifugo nchini ambao unatilia mkazo matumizi ya maji katika kilimo, matumizi ya mbegu bora, mbolea, dawa, masoko na miundombinu imara kuweza kufikisha mazao kwa walaji.  Jitihadi hizi ndiyo zitakazowezesha maisha ya Watanzania kuinuka na kuimarika.

Wilaya ya Bunda pia itaingizwa katika mpango wa kupewa ruzuku ya mbolea na mbegu ili kuongeza na kukuza kilimo.

Wilaya ya Bunda pia ina tatizo la maji safi na salama ambapo Rais amewaeleza wananchi kuwa tayari mradi mkubwa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia umeshaanza ambapo wilaya itapata maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria na pia tatizo la barabara za Bunda zimeshafanyiwa tathmini na kuingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi mwaka huu na ujezi utaanza mara moja.

Ambapo Wilaya itapata maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria na pia tatizo la barabara za Bunda zimeshafanyiwa tathmini na kuingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi mwaka huu na ujenzi utaanza mara moja.  Rais ameondoka Bunda na kuelekea Nansio Ukerewe, ambapo atazindua Mradi wa Umeme Vijijini.

 

Imetolewa na

PREMI KIBANGA,

Bunda,

Mara.

05/07/2010