DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewahimiza
wana-CCM kutumia mtandao wao mkubwa na mpana wa kisiasa kuhakikisha kuwa
wananchi wanajitokeza kwa wingi kukipigia kura chama hicho Oktoba 31, mwaka
huu, 2010.
Aidha, Mheshimiwa Kikwete amewatahadharisha wana-CCM dhidi ya hisia za
kudharau wapinzani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hata
Vile vile, Mheshimiwa Kikwete amewapongeza
Wazanzibari kwa kufanikisha kura ya maoni ambayo imefungua njia ya kuundwa kwa
Serikali ya Umoja visiwani humo.
Mheshimiwa Kikwete pia amekemea tabia ya
baadhi ya vyama vya siasa kutumia matusi, ubabe na vikundi vya wahuni wakati wa
kampeni kwa nia ya kuruvuga mikutano ya vyama pinzani ama kuwatukana wanasiasa
wapinzani.
Rais Kikwete ameyaeleza hayo leo, Jumatatu,
Agosti 2, 2010 wakati alipowahutubia mamia kwa mamia ya wana-CCM na wananchi
wengine kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Mheshimiwa Kikwete amesema: “CCM ina
mtandao mkubwa na mpana
Kuhusu dharau kwa vyama vya upinzani,
Mheshimiwa Kikwete amesema: “Tusidharau wapinzani wetu hata
“Tuache kudharau adui. Tuthibitishe nguvu
zetu kwenye kura. Tunadi sera zetu. Wenzetu watapimwa kwa maneno
Kuhusu kura ya maoni ya Zanzibar,
Mheshimiwa Kikwete amesema: “Napenda kuwapongeza Wa-Zanzibar kwa uamuzi wao wa
busara wa juzi kwa kuamua kuchagua Serikali ya Umoja. Najua kuwa kila chama cha
siasa hupenda chenyewe kushinda uchaguzi na kuunda Serikali, lakini yapo
mazingira ambako lazima ushinde na mwenzio. Na hiyo ndiyo hali iliyoko
Mheshimiwa Kikwete ameeleza kuwa
makubaliano ya kuunda Serikali ya Umoja yalikuwemo kwenye hata Mwafaka wa
kwanza kati ya CCM na CUF. Pia ameeleza kwa urefu uzoefu wa nchi nyingine katika
uundaji wa serikali za namna hiyo ikiwa ni pamoja na katika nchi za DRC,
Kuhusu tabia ya matusi, Mheshimiwa Kikwete
amesema kuwa yeye binafsi hasumbuliwi na ushindani wa kawaida wa kisiasa. “Wapo
watu watatusema. Hili halinipi wasiwasi hata kidogo kwa sababu hata tufanyeje
kuna watu wasiotupenda na watatusema tu. Na watu hawa muhimu wawepo ili
demokrasia yetu iweze kukua. Hivyo tunahitaji kuwepo vyama vingi na vyenye
nguvu.”
Lakini ameongeza: “Linalonisumbua mimi ni tabia
ya kutukanana, kufanyiana fujo, kuandaa vikundi vya wahuni kuvunja mikutano ya
wenzio, kupiga watu badala ya watu kunadi sera zao na kuwaachia wananchi nafasi
ya kupima na kuamua wenyewe. Kuna watu wasiojua bado kuwa fujo hufukuza kura.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
02
Agosti, 2010