DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

RAIS KIKWETE AISHUKURU CHINA KWA UWANJA

 

Na Mwandishi Maalum,

 

 

TANZANIA imeshukuru China kwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa soka uliojengwa mjini Dar es Salaam.

 

Tunawashukuru sana kwa uwanja,” amesema Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Alhamisi, Septemba 18, 2008) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China.

 

Katika mazungumzo yake na ujumbe huo kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Dar es Salaam (KIA), Rais Kikwete amemwomba kiongozi wa ujumbe huo, He Yong, kuwasilisha shukurani zake hizo kwa Rais wa China, Hu Jintao.

 

He Yong, ambaye ni Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China aliongoza ujumbe wa chama hicho ambao umefanya ziara ya siku tatu nchini kwa mwaliko wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

Ziara hiyo ya ujumbe wa China nchini ni sehemu ya ziara ya Afrika ambako ujumbe huo unatembelea Afrika Kusini, Uganda, Gabon na Nigeria.

 

Ameuambia ujumbe huo Rais Kikwete, “uwanja ni mzuri sana. Hata Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limevutia na uwanja huo. Ni matarajio yetu kuwa mwaka 2010 baadhi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Kombe la Soka Duniani huko Afrika Kusini, zitafanyia mazoezi kwenye uwanja huo.”

 

Fainali zijazo za Kombe la Soka la Dunia (FIFA Senior World Cup Finals) zimepangwa kufanyika Afrika Kusini mwaka 2010 na nchi jirani na Afrika Kusini zinaratajiwa kunufaika kwa kuwa wenyeweji wa mazoezi ya timu hizo 32 zitakazoshiriki fainali hizo.

 

Mwambie Rais Jintao kuwa tunashukuru sana kwa kutuunga mkono katika hilo. Asanteni sana kwa urafiki wenu wa kindugu kabisa,” amesema Rais Kikwete.

 

Naye He Yong amesema kuwa atawasilisha shukurani hizo kwa Rais Jintao na kuongeza: “Siku zote tumekuwa na hisia za urafiki wa pekee kwa wananchi wa Tanzania, kwa sababu mmetuunga mkono kwa mengi katika miaka 44 tokea tuanzishe uhusiano kati ya mataifa yetu.”

 

 

 

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

18 Septemba, 2008