UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Ijumaa, Mei 14, 2010, amekutana na kufanya mazungumzo na Mtoto wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mheshimiwa Prince Sultan Bin Muhammed Bin Saud Al-Kabeer.

 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete na mgeni wake walijadili mipango ya Mtoto huyo wa Mfalme kuwekeza katika kilimo nchini kwa kushirikiana na taasisi za Serikali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Idara ya Magereza.

 

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Ulinzi na Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dk. Hussein Mwinyi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bwana Emmanuel Ole Naiko; na wakuu na maofisa wengine waandamizi wa JKT na Magereza.

 

Prince Al Kabeer ambaye yuko katika ziara ya Tanzania amemwambia Rais Kikwete kuwa kwa mujibu wa mipango yake, uwekezaji huo katika kilimo utaanza kidogo na kupanuka kwa kadri mambo yanavyokuwa mazuri.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu

DAR ES SALAAM.

 

14 Mei, 2010