DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa
Taarifa iliyotolewa leo
Jumanne tarehe 20 Julai, 2010 Jijini
Taarifa hiyo imewataja walioteuliwa kuwa ni pamoja
na Bwana Ngosi C.X. Mwihava, Kamishna Msaidizi (Nishati Mbadala) katika Wizara ya Nishati
na Madini kuwa Naibu Katibu
Mkuu katika Ofisi ya Makamu
wa Rais.
Aidha, kwa mujibu wa
taarifa ya Bwana Luhanjo, Rais Kikwete
amewateua Balozi Herbert E.
Mrango ambaye ni Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kanda katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuwa
Naibu Katibu Mkuu katika Wizara
ya Miundombinu; Balozi Rajab Gamaha ambaye ni Balozi
wa Tanzania nchini Uganda kuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, na Bwana Mbogo Futakamba, Mkurugenzi wa Umwagiliaji na Ufundi ambaye
sasa anakuwa Naibu Katibu Mkuu
katika Wizara ya Maji na
Umwagiliaji.
Katika Uteuzi huo, Rais
Kikwete pia amewateua Dk. Yohana L. Budeba ambaye ni
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) kuwa Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi, na Bibi
Maria H. Bilia ambaye ni Katibu Tawala
wa Mkoa wa
Kagera kuwa Naibu Katibu Mkuu
katika Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi.
Aidha, Rais Kikwete amewateua
Bibi Nuru H.M. Mlao ambaye kwa
sasa ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Arusha
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii;
Bwana Hussein A. Katanga ambaye ni
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Morogoro kuwa Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, na
Bwana Job D. Masima ambaye ni Mkurugenzi katika
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa Naibu Katibu
Mkuu katika Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
20
Julai, 2010