UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Mgombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, Jumatano, Agosti 18, 2010, ametoa tamko rasmi kuthibitisha kuwa maelezo yote aliyoyatoa kwenye fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea urais ni sahihi.

 

Mheshimiwa Kikwete ametoa tamko hilo kwa kujaza fomu maalum ya tamko katika shughuli fupi iliyofanyika katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania mjini Dar es Salaam mbele ya Jaji Mkuu, Jaji Augustino Ramadhani aliyemshuhudia na kuthibitisha kuwa tamko hilo limetolewa mbele yake.  Fomu hizo hutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

Mheshimiwa amelazimika kutoa tamko hilo ili kutimiza matakwa ya Sheria ya Uchaguzi, ambayo ni Sheria Nambari Moja ya mwaka 1985.

 

Mheshimiwa Kikwete, akiwa amefuatana na Mgombea Mwenza wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal ambaye alipanda naye gari moja, amewasili Mahakama ya Rufani kwenye makutano ya Barabara za Sokoine na Ohio kiasi cha saa tano na dakika 20 asubuhi.

 

Alikwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Mahakama hiyo ambako yeye na Dk. Bilal walijaza fomu za kutoa tamko, shughuli ambayo ilichukua muda mfupi na katika muda wa dakika 10 Mheshimiwa Kikwete aliondoka kurejea Ikulu.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

18 Agosti, 2010