UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Rais Kikwete na
Mama Salma Kikwete waliwasili kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura cha
Shule ya Msingi Msoga, kijiji cha Msoga, kiasi cha saa nne asubuhi, na
kupokelewa na msimamizi wa kituo hicho, Ndugu Diana Frederick.
Kwenye uchaguzi
mkuu uliopita wa mwaka 2005, Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete walipiga kura
kwenye mji mdogo wa Chalinze wilaya hiyo hiyo ya Bagamoyo lakini zamu hii
wameamua kujiandisha, ili waweze kupiga kura kijijini kwao.
Rais Kikwete na
Mama Salma Kikwete wamejiandikisha katika kituo kipya kufuatia kuanza kwa zoezi
la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwa Kanda ya Mashariki.
Uboreshaji wa Daftari
la Wapigaji Kura kwa Kanda ya Mashariki ulianza Jumatatu ya wiki hii, Machi
Mosi, 2010, na umepangwa kumalizika keshokutwa, Machi 6, 2010.
Chini ya uboreshaji
huo, wanaandikishwa wapigaji kura wapya, walioamua kubadilisha vituo vyao vya
kupiga kura, ama waliopoteza shahada zao za kupigia kura.
Kufuatia hatua yake
hiyo, Rais Kikwete amerudia tena wito wake kwa wananchi wenye sifa za kupiga
kura kutumia nafasi ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa kujiandikisha
kwa mara ya kwanza kama wapigaji kura, na kwa wale waliopoteza shahada zao
kujiandikisha upya, ili wapate sifa za kutumia haki yao ya kupiga kura katika
Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
04 Machi, 2010