UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete jana
(21 Septemba, 2011) amepokea
Tuzo Mbili Maalum kwa mchango
wake mkubwa katika Afya ya Mama Mjamzito
na Watoto kwa ujumla kutoka
taasisi mbili tofauti mjini New York.
Tuzo
ya kwanza imetolewa na Taasisi
ya Kijamii ya Umoja wa
Mataifa (UN
Foundation) na kukabidhiwa
kwa Rais na Makamu wa
Rais wake anayeshughulikia
sera ya Umma Bw. Peter Yeo.
Rais
amepokea Tuzo ya pili katika
makao makuu ya Soko la Hisa
la Marekani (National
Association of Securities Dealers Automated Quotations) kwa kifupi NASDAQ ambalo ni soko
la pili kwa ukubwa duniani baada ya lile
la New York. Rais
amekabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais
wa NASDAQ Bw. David Wicks.
Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Rais
amepewa heshima maalum ya kugonga
kengele kuashiria mwisho wa
biashara kwa siku hiyo.
Akipokea
tuzo hizo mbili maalum, Rais
ameelezea changamoto zinazoikabili sekta ya Afya nchini
Tanzania na Afrika kwa ujumla
na kuzishukuru nchi na taasisi
mbalimbali ambazo zinaunga mkono juhudi za kupunguza
matatizo ya afya ya mama mjamzito.
“Si sahihi
kwa mama mjamzito
kufariki wakati anampa uhai binadamu
mwingine, uzazi unatakiwa kuwa shughuli ya furaha
na sio huzuni
na ndiyo maana tumetoa kipaumbele
kwenye afya ya mama mjamzito kwenye ajenda yetu
ya Afya” Rais amesema.
Rais
amewaeleza wageni waalikwa ambao katika hadhara zote mbili wametoka
katika nchi na taasisi
mbalimbali kuwa kati ya vitu
ambavyo serikali ya Awamu ya
Nne imeamua kutoa kipaumbele katika kuongeza huduma za afya
ya uzazi kwa kujenga zahanati
na kuzipandisha daraja zilizokuwepo.
Serikali
pia inaajiri wakunga na
wataalamu zaidi wa Afya na
kuongeza mafunzo katika sekta hiyo.
Juhudi
zingine ni
pamoja na kutoa huduma za
Mpango wa Uzazi bure na
kutoa vifaa vya kujifungulia kwa akina mama wanaohudhuria kliniki.
“Vifaa hivi ni maalum kwa ajili
ya kuwasaidia akina mama wakati wa kujifungua, na tuna amini kuwa
kwa kufanya hivi wanawake wengi
zaidi watahudhuria kliniki na kuwapa
motisha wa kujifungulia katika taasisi zetu za
afya”. Rais ameeleza.
Kutokana
na juhudi hizo takwimu zinaonyesha
kupungua kwa vifo vya akina
mama wajawazito na wakati
wa kujifungua kutoka 8,000 kwa mwaka 2005 hadi 6,000 mwaka jana.
“Upungufu wa vifo
2,000 ni hatua nzuri katika muda
mfupi lakini bado hairidhishi sana, tunaweza kupunguza zaidi na hilo ndiyo
lengo letu kwani hatutaki kuona mwanamke yeyote anakufa kutokana na ujauzito
au wakati wa kujifungua”. Rais amesema.
Mbali
na shughuli hizo, Rais amekutana
na kufanya mazungumzo na Rais
wa Slovenia Dr. Danilo
Turk, Makamu Waziri Mkuu wa Luxembourg Bw. Jean Asselborn na Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa Bw.
Ban Ki Moon na Waziri wa Maendeleo wa
Uingereza Bw. Andrew
Mitchell.
Leo tarehe 22 Septemba, 2011, Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
MWISHO.
Imetolewa
na Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari
wa Rais Msaidizi,
New York.
Marekani.
22
Septemba, 2011