UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo
asubuhi amepokea hati za utambulisho
kutoka kwa mabalozi wa Australia, Finland,
Mexico na Misri.
Mabalozi
Geoffrey Peter Tooth wa Australia na
Balozi Luis Javier Campuzano
wa Mexico watakuwa na makazi yao
jijini Nairobi wakati Balozi Sinikka Antila wa Finland na Hossam Eldin
Moharam wa Misri watakuwa na makazi yao
hapa jijini Dar-Es-Salaam.
Mapema
kabla ya kupokea Hati za
Utambulisho za mabalozi hao Rais
Kikwete amekwenda kenye makazi ya
balozi wa Cuba hapa nchi, ambapo
ametia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Makamu wa Rais
wa Cuba, Jenerali Julio
Casas Regueiro.
Wakati
huo huo Rais
Kikwete mchana huu anatarajiwa kuelekea Nairobi , Kenya kwa ziara ya kikazi
ya siku moja,
kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais
Mwai Kibaki wa Kenya.
Akiwa
Nairobi, Rais Kikwete anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa
Kimataifa kuhusu Ukame Ulioathiri Nchi za Pembe
ya Afrika.
Mkutano
huo utakaoongozwa na Rais Kibaki, unatarajiwa pia kuhudhuriwa na viongozi kutoka
Djibouti, Ethiopia, Somalia, Uganda, Sudan na Sudan Kusini.
Mkutano
pia utahudhuriwa na viongozi wa
Taasisi za Kimataifa ambazo ni Umoja wa
Afrika (AU) Umoja wa Mataifa
(UN), Mwenyekiti wa Benki ya Dunia
na Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Umoja
wa Mataifa.
Rais
Kikwete anatarajiwa kurejea kesho mara
baada ya kikao hicho kumalizika.
Mwisho
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu
Dar
es Salaam.
08 Septemba, 2011