UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone:
255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Aidha,
Rais Kikwete ametoa shukurani za pekee kwa wakazi wa Dar es Salaam
waliojitokeza kwa wingi kuwalaki wageni wa mkutano huo na kuwa wavumilivu kwa
kipindi chote cha mkutano pamoja na usumbufu wa hapa na pale.
Rais
Kikwete pia ametoa changamoto ya
Rais
Kikwete alikuwa akizungumza jana, Ijumaa, Mei 14, 2010, katika halfa ya chakula
cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza watu waliokuwa mstari wa
mbele katika kufanikisha mkutano huo wakiongozwa na Kamati ya Taifa ya
Maandalizi ya mkutano huo chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Kiongozi, Ndugu
Philemon Luhanjo.
Rais
Kikwete aliwaambia washiriki wa chakula hicho kwenye Hoteli ya Movenpick mjini
Dar es Salaam:
“Ndugu
zangu, nimeona ni vyema tukutane, tupate chakula cha usiku pamoja kwa ajili ya
kuwapongeza kwa kazi mliyoifanya ya kuhakikisha kwamba Mkutano wa Kimataifa wa
Uchumi Duniani Kuhusu Afrika unafanyika nchini kwetu kwa mafaniko makubwa.”
Akiwashukuru
wakazi wa Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema: “Shukurani za pekee ziwafikie
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuwalaki wageni wetu,
walikuwa wavumilivu kwa kipindi chote cha mkutano, najua kulikuwa na usumbufu
wa hapa na pale hasa kwa upande wa barabara. Lakini mlivumilia kwa mapenzi ya
nchi yenu na ukarimu wetu kwa wageni wetu. Nawashukuruni
Rais
Kikwete pia ameyashukuru makundi maalum kwa mchango maalum katika kufanikisha
mkutano huo ikiwa ni pamoja na madaktari na wauguzi, vyombo vya ulinzi na
usalama na hasa askari wa usalama barabarani, na vikundi vya burudani
vilivyotumbuiza katika halfa ambayo Rais aliwaandalia wageni wa mkutano huo.
Rais
pia ametoa shukurani maalum kwa wafadhili wa mkutano huo yakiwamo makampuni ya
Seregenti Breweries, Bakhresa Group, mabenki ya NMB, CRDB na NBC, Precision
Air, Barrick Gold Mine na Benki Kuu ya
Rais
pia ameshukuru uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Julius K. Nyerere, mahoteli
yaliyowapokea na kuwahudumia wageni, vyombo vya habari na makundi mengine yote
yaliyotoa mchango maalum wakati wa mkutano huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Mei, 2009