UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz

Website:  www.mawasilianoikulu.go.tz  

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Juni 6, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Utamaduni, Michezo na Utalii wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Dkt. Choung Byoung Gug.

 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, viongozi hao wawili wamezungumzia uhusiano kati ya Tanzania na Korea na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika Nyanja mbalimbali.

 

Miongoni mwa mambo mengine, Mheshimiwa Gug amemwelezea Rais Kikwete mipango ya nchi hiyo ya kutaka kuitangaza Mbuga ya Wanyama ya Serengeti ili kuweza kuvutia watalii zaidi wa Korea kutembelea Tanzania.

 

Mheshimiwa Gug pia amemwelezea Rais Kikwete kuhusu mipango ya nchi hiyo ya kuisaidia Tanzania katika kujenga maktaba katika shule za msingi hasa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kuwafundisha walimu namna bora zaidi ya kutumia maktaba hizo.

 

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

06 Juni, 2011