DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais Kikwete apokea ripoti ya awali ya milipuko ya Mlima Oldonyo Lengai

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatano, Januari 28, 2009, alipokea ripoti ya awali ya milipuko ya mara kwa mara ya jivu la volkano kutoka kwenye  kwenye Mlima wa Oldonyo Lengai katika Mkoa wa Arusha kutoka kwa watalaam wa masuala ya volkano wa Marekani.

 

Ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Rais Kikwete na Mshauri wa Sayansi ya Miamba kutoka Ofisi ya Mpango wa Marekani wa Misaada ya Nje ya Maafa (VDAP) cha Mamlaka ya Maendeleo ya Kimataifa, Gari Mayberry wakati mtaalam huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais. Ikulu, Dar es Salaam.

 

Maybeery alimwambia Rais Kikwete kuwa ripoti hiyo ni ya awali tu na uchunguzi zaidi utahitaji kuweza kuthibitisha baadhi ya mambo ambayo yamegunduliwa katika uchunguzi huo wa awali.

 

VDAP ilifanya uchunguzi huo kuhusu milipuko ya mara kwa mara ya volkano katika Mlima Oldonyo Lengai kufuatia ombi la Serikali ya Tanzania kupitia kwa aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini, Mark Green ambaye ameondoka nchini majuzi baada ya kuwa amemaliza muda wake wa utumishi.

 

Ripoti hiyo ya awali imegundua masuala matano kuhusu milipuko hiyo na inatoa mapendekezo ya aina mbili – manane ya muda mfupi na mawili ya muda mrefu.

 

Mlima wa Oldonyo Lengai ulioko chini ya Mamlaka ya Eneo la Hifadhi la Ngorongoro (NCCA) ulilipuka mara kwa mara hasa mwaka juzi na kufuatia hali hiyo, Serikali ya Tanzania iliomba msaada kutoka Marekani wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu milipuko hiyo na madhara yake.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

29 Januari, 2009