DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BAADHI ya makubaliano makuu yaliyofikiwa kwenye kikao cha leo, Jumanne,
Februari 24, 2009, Ikulu,
(a)
Kwamba msimamo wa Serikali
kupiga marufuku uuzaji wa magogo
nje ya nchi
ubakie pale pale kwa sababu una
manufaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja
na kuwashawishi wafanyabiashara wa bidhaa za mbao
kuuza nje bidhaa ambazo tayari
zimeongezwa thamani.
(b)
Kwamba hatua zaidi zichukuliwe kuimarisha usalama wa misitu nchini
kwa kuajiri walinzi wa misitu
zaidi, kuwabana na kuwadhibiti maofisa wa Serikali
waliopewa jukumu la kusimamia usalama huo lakini siyo
waaminifu, kusisitiza miiko ya utumishi
wa umma katika
usalama wa misitu, na kuendeleza
elimu ya umma kuhusu usalama
wa misitu.
(c)
Kwamba juhudi ziongezwe katika kampeni ya uhamasishaji
wa kupanda
miti nchini kwa sababu liko
pengo kubwa kati ya miti
inayopandwa na ile inayokatwa kila mwaka. Imeelezwa
kuwa utafiti uliofanywa mwaka 1992 unaonyesha kuwa wakati zinapandwa hekta 25,000 za miti, kiasi cha hekta 92,000 zinakatwa kila mwaka.
(d)
Kwamba Wizara ya Maliasili na
Utalii ianze programu ya haraka
ya kutenga maeneo maalum kwa
ajili ya kupanda miti inayokua
haraka kama njia ya kuongeza
kasi ya kupanda
miti, kujenga akiba ya misitu
kwa ajili ya matumizi ya
nishati hasa kwa wakazi wa
mijini, na hivyo kulinda misitu
ya asili na ya kisasa
ili isindelee kukatwa.
(e)
Kwamba uongozi wa Wizara
ya Maliasili na Utalii usimamie
na udhibiti zaidi sekta ya
misitu kwa lengo la kuiwezesha sekta hiyo kuongeza
pato la taifa kutokana na mazao
ya sekta hiyo.
(f)
Kwamba jitihada ziendelee katika kufanya tafiti kutafuta nishati mbadala badala ya matumizi ya
kuni, na
pia kutekeleza matokeo ya tafiti
ambazo tayari zimefanyika na kuthibitisha kuwa matumizi yanaweza kupunguza matumizi ya kuni nchini.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24
Februari, 2009