DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

 

Rais Kikwete amtumia salamu za rambirambi Rais Kibaki wa Kenya

 

Na Mwandishi Maalum, Addis Ababa, Ethiopia

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Rais Mwai Kibaki wa Kenya salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu zaidi ya 140 katika ajali mbili za moto zilizotokea nchini humo majuzi.

 

Katika salamu hizo ambazo zilikabidhiwa jana, Jumanne, Februari 3, 2009, kwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya, Moses Wentangula, mjini Addis Ababa, Ethiopia, Rais Kikwete ameeleza mshituko na huzuni yake kubwa kufuatia vifo hivyo.

 

Amesema Rais Kikwete katika rambirambi hzo kwa Rais Kibaki: “Nimepokea kwa mshituko mkubwa na huzuni nyingi habari za vifo vya zaidi ya watu 145 vya wananchi wako kutokana na ajali mbili mbaya za moto katika Molo na Nairobi.”

 

Watu wengine wengi pia wameumia na mali nyingi imeharibiwa ama kuteketezwa katika kila kinachoelezwa kuwa miongoni mwa ajali mbaya zaidi katika Bara la Afrika, amesema Rais Kikwete na kuongeza:

 

Kwa niaba ya watu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nakutumia wewe, na kupitia kwako, familia za wafiwa wote, na watu wote ndugu zetu wa Kenya, salamu zangu za moyoni kabisa za rambirambi na za majonzi makubwa.”

 

Katika rambirambi hizo, Rais Kikwete pia amewatakia wote walioumia katika ajali hizo kupona haraka.

 

Salamu hizo za rambirambi zilikabidhiwa kwa Waziri Wetangula kwa sababu Rais kibaki, ambaye kama alivyokuwa Rais Kikwete, alikuwa mjini Addis Ababa kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), alilazimika kuondoka haraka kurejea nyumbani kwa sababu ya ajali hizo.