UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu
wa Mkoa
wa Pwani Mhe. Hajat Amina
Mrisho kutokana na ajali
mbili tofauti za barabarani zilizotokea
mwishoni mwa wiki.
Ajali ya kwanza iliyohusisha basi aina ya
Toyota Coaster na lori lenye tela,
ilipoteza maisha ya watu 14 na
kujeruhi wengine 12. Ajali hiyo ilitokea eneo
la Mbala-Vigwaza katika Wilaya ya Bagamoyo
Mkoani Pwani kufuatia basi hilo kuligonga kwa nyuma lori
lenye tela.
Ajali nyingine iliyotokea siku hiyo hiyo
ilihusisha malori matatu ambayo yaligongana
katika eneo la Ubena – Zomozi Wilayani Bagamoyo katika mkoa huo
huo wa
Pwani ambapo watu watatu walipoteza
maisha na wengine sita kujeruhiwa.
“Kupotea kwa maisha
ya watu hao
17 ni hasara kubwa kwa Taifa
kutokana na umuhimu waliokuwa nao wakati wa
uhai wao kwa maendeleo na
ustawi wa nchi yetu”, amesema
Rais Kikwete.
Amesema kupoteza maisha kwa watu
hao kumemhuzunisha zaidi kwa kuona
kwamba ni siku chache tu
zilizopita tangu Taifa lipoteze maisha ya wasanii
14 wa muziki wa Taarab katika
ajali ya barabarani.
Kupitia kwa Mkuu
huyo wa Mkoa,
Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa
familia za watu wote waliofariki
katika ajali zote mbili huku
akimwomba Mwenyezi Mungu azilaze mahali
pema peponi roho za marehemu
hao.
Rais Kikwete amesema anawahakikishia wafiwa wote kuwa yuko
pamoja nao katika msiba huo
mkubwa, na
amewaomba wawe wavumilivu na wenye
subira katika kipindi hiki kigumu
cha maombolezo ya wapendwa wao.
Aidha Rais Kikwete anawaombea
kwa Mwenyezi
Mungu majeruhi wote waweze kupona
haraka na kurejea katika hali zao za
kawaida na kuungana tena na
ndugu, jamaa na marafiki zao
na kuendelea na maisha kama
mwanzoni.
Rais Kikwete amezikumbusha mamlaka zote zinazohusika
na usimamizi
wa usalama barabarani kuongeza jitihada za kusimamia
usalama wa watu wanaosafiri, ili Taifa lisiendelee
kupoteza nguvu kazi yake kutokana
na ajali za barabarani.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
29 Machi, 2011