DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
|
Telephone:
255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za Rambirambi
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake
Tanzania, Bibi Sophia Simba,
kufuatia kifo cha mmoja wa wanachama
wake hodari Bibi Rhoda Kahatano aliyefariki usiku wa kuamkia
leo nyumbani kwake Bunju A, jijini Dar-Es-Salaam.
Katika
salamu hizo Rais Kikwete amesema
amemfahamu na
kufanya naye kazi katika chama
na serikali na kumuelezea kuwa
mwananchama dhabiti, aliyeshirikiana vyema na wenzake na
muwajibikaji mkubwa.
“Alikwua
nguzo imara katika kusimamia masuala ya chama
na serikali na muwajibikaji ambaye anakumbukwa wakati wote kwa ushirikiano na upendo mkubwa kwa
wenzake siku zote”. Rais amesema
“Tutamkumbuka kwa kupenda kutoa
ushauri, ushirikiano, upendo na ucheshi
kwa watu wote na wakati
wote” Rais amesema na
kumuomba Mwenyekiti wa UWT, amfikishie rambirambi zake kwa Mume, watoto
na wana familia
ya Marehemu Rhoda Kahatano kwa kuondokewa
na mpendwa wao.
Marehemu
Rhoda Kahatano alizaliwa Tukuyu, Mbeya tarehe
15 Desemba, 1941. Aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya mkoani Kagera kabla
ya kuwa Mbunge
wa Viti Maalum
kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kutoka mwaka 1995 hadi 2000.
Amekuwa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mjumbe
wa UWT katika kipindi cha uhai wake.
Ameacha
mume, watoto na wajukuu.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
18
Agosti, 2010