UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JAKAYA
MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia salamu za rambirambi
Mkuu wa
Mkoa wa Pwani,
Mhe. Hajat Amina Mrisho kufuatia
vifo vya watu 10 na
wengine 19 kujeruhiwa kutokana na ajali
ya barabarani iliyotokea tarehe 14 Septemba, 2011 katika kijiji cha Mwindu wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa
Pwani baada ya basi la Kampuni
ya Grazia Safari’s kupinduka likitokea Songea kuelekea Dar es Salaam.
Nimeshtushwa,
na kusikitishwa
sana kwa Taifa letu kupoteza,
kwa mara nyingine, roho za Watanzania wenzetu
10 waliofariki kutokana na ajali mbaya
ya barabarani katika eneo la mkoa wako,” amesema
Rais Kikwete katika salamu zake
na kuongeza,
“Naomba unifikishie salamu zangu za
pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika
ajali hii mbaya. Nawahakikishia kwamba nipo pamoja
na familia hizo katika kipindi
chote cha maombolezo kwani msiba huu
ni wetu sote.”
Rais Kikwete amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azilaze pema peponi
roho za marehemu
wote. Aidha, amesema anawaombea kwa
Mola wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo wapone
haraka ili waweze kuungana tena na familia
zao na kuendelea
na maisha yao ya kawaida.
Amesema kutokana na kukithiri
kwa ajali za barabarani ambazo
zimeendelea kulinyang’anya Taifa nguvukazi muhimu kwa maendeleo
ya nchi yetu,
vyombo vyote vinavyohusika na usalama wa barabarani
havina budi kusimamia kwa karibu
mwenendo wa vyombo vya usafirishaji
wa abiria ili kuepusha kutokea
kwa ajali zaidi za barabarani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
15
Septemba, 2011