UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz

Website:  www.mawasilianoikulu.go.tz  

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaandikia barua Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha kuwataka kuziwakilisha bungeni ifikapo tarehe 12 Aprili, mwaka huu ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Serikali  juu ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Hesabu za Serikali Kuu,  za  Mashirika ya Umma na Ukaguzi wa Ufanisi kwa mwaka 2009/10 kama ilivyo kikatiba.

 

Tayari Mkaguzi Mkuu ameziwakilisha ripoti hizi kwa Rais, jana mchana (29 Machi, 2011) kama  ilivyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyorekebishwa mwaka 2005, kifungu cha 28 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma namba 11 ya mwaka 2008.

 

Kwa Mujibu wa Sheria Ripoti hizi zinatakiwa kuwakilishwa kwa Rais kabla ya tarehe ya mwisho wa mwezi wa Machi, na Rais anatakiwa kuwaandikia mawaziri wanaohusika mapema iwezekanavyo ili kuweza kuwasilishwa kwenye kikao  cha bunge linalofuata baada ya hapo.

 

Ripoti hizo zinahusu ukaguzi wa fedha za Serikali za Mitaa, Serikali Kuu na za Mashirika ya Umma. Ripoti pia zimekagua ufanisi wa utendaji  wa Wizara ya Miundombinu na TANROADS katika kusimamia na ujenzi wa barabara nchini.

 

 

 

Ripoti zimebainisha kuwa bado kuna mapungufu na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kurekebishwa na pia Mkaguzi Mkuu ametoa  mapendekezo muhimu ambayo yanalenga katika udhibiti na matumizi bora ya fedha na rasilimali za nchi hii ambayo Rais ameyaafiki.

 

Rais amemshukuru na kumpongeza Mkaguzi Mkuu, Bw. Ludovick Utouh kwa kazi yake nzuri na makini na kumtaka aendelee na kuwachukulia hatua wale wote wanaokiuka taratibu na kutumia fedha za Umma vibaya  na kueleza kuwa lazima viongozi na watumishi wa serikali kuzingatia taratibu zilizopo na kutambua kuwa serikali haiwezi kuendeshwa kama haikusanyi mapato yake vizuri.

 

Mwisho.

 

Imetolewa na:

 

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Ikulu,

DAR ES SALAAM

 

30 Machi, 2011