UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA POLE ZA RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGAO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT.
JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
ametuma salamu za pole kwa watu
walioathiriwa na mafuriko mkoani Morogoro kwa kukosa
mahali pa kuishi baada ya nyumba
zaidi ya 200 kuharibiwa vibaya na mafuriko hayo
kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika Milima ya
udzungwa na Mahenge kati ya
tarehe 19 na 25 Aprili, 2011.
Katika salamu zake hizo
za pole kupitia kwa Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro,
Luteni Kanali Mstaafu, Mheshimiwa Issa Machibya, Rais Kikwete ameelezea
kusikitishwa kwake na madhara makubwa
waliyoyapata watu hao hususan wa
maeneo ya Mbingu na Ifakara
kutokana na
mafuriko hayo ambayo pia yameharibu
kwa kiasi kikubwa miundombinu na kuathiri zaidi
ya ekari 600 za mazao hususan
zao la mpunga ambalo ni tegemeo
lao kubwa kwa chakula na
biashara.
Rais Kikwete amesema Serikali yake inafanya
kila linalowezekana kuhakikisha kwamba wananchi wote walioathiriwa
na mafuriko
hayo wanapatiwa misaada stahiki ya hali na
mali ili kuwawezesha kurejea katika maisha yao
kama ilivyokuwa kabla ya kutokea
kwa mafuriko hayo. Wakati huo huo,
Rais Kikwete amepongeza hatua za awali na za
haraka zilizochukuliwa na uongozi wa
Mkoa wa Morogoro
kunusuru maisha ya wananchi walioathiriwa
na mafuriko hayo, huku akihimiza
mamlaka zinazohusika na udhibiti wa
maafa na wadau wengine kushirikiana
kwa karibu na uongozi wa
Mkoa huo kunusuru maisha ya wananchi hao
na kuangalia namna ya kuepukana
na hali hiyo
kwa siku za usoni.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
27
Aprili, 2011