UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz

Website:  www.mawasilianoikulu.go.tz  

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE

 

                Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa John Guninita kufuatia kifo cha Mzee Athumani Mwinyimvua, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kilichotokea Alhamisi, Mei 19, 2011 kutokana na ugonjwa wa Kansa ya Koo.

 

                Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amemwelezea Marehemu Mwinyimvua kama kiongozi aliyetumia muda mwingi wa uhai wake kujenga mahusiano mazuri ndani ya jamii ya Watanzania.

 

Rais amesema kuwa alimfahamu vyema Marehemu Mzee Athumani Hassan Mwinyimvua ambaye amefariki akiwa na miaka 81 tangu enzi ya uhai wake kama nguzo imara na tegemeo kubwa la Chama Cha Mapinduzi kutokana na ushauri muhimu aliokuwa akiutoa uliolenga mara zote katika kukiimarisha chama.

 

                Kifo cha Mzee Athumani Hassan Mwinyimvua ni pigo kubwa siyo tu kwa familia yake, bali pia kwa wana – CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam na kote kwingineko nchini. Kwa hakika tumempoteza mtu muhimu sana kwa uhai wa chama chetu,  amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

 

                Aidha Rais Kikwete amemuomba Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam kumfikishia salamu zake za pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu Mzee Athumani Hassan Mwinyimvua kwa kumpoteza kiongozi na mshauri muhimu wa familia.

 

                Rais Kikwete amesema anamuomba Mola awajalie moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewahakikishia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huo mkubwa.

 

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiano ya Rais,

Ikulu

DAR ES SALAAM.

 

21 Mei, 2011