DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Mheshimiwa William Lukuvi kutokana na vifo vya watu 10
waliopoteza maisha kwa ajali ya barabarani baada ya lori kubwa la mafuta lenye
tela kugongana na basi dogo la abiria aina ya Hiace na hatimaye kulilalia na
kusababisha watu wote waliokuwemo kwenye basi hilo kufariki. Ajali hiyo ilitokea eneo la Kibamba nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kupitia
kwa Mheshimiwa Lukuvi, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa wote
walipoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya. “Kupitia kwako, ninatuma salamu
za rambirambi kwa watu wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali
hiyo mbaya,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake, na kuongeza, “ninaelewa
fika ni kwa kiasi gani hivi sasa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu
wanaelemewa na huzuni kubwa na majonzi baada ya kuwapoteza wapendwa wao”.
Amewaomba
wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na ujasiri wakati huu mgumu wa maombolezo
ya vifo vya ndugu, jamaa na marafiki zao na amemuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi.
Katika
salamu zake hizo, Rais Kikwete amezisisitizia mamlaka zinazohusika na Sheria ya
Usalama Barabarani kuisimamia kikamilifu sheria hiyo ili Taifa lisiendelee
kupoteza watu wake kutokana na kukiukwa kwa sheria hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
26 Machi, 2010