DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA
RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa
“Ninaelewa huzuni kubwa waliyo nayo
waliofikwa na
msiba huo, hivyo kupitia kwako
wewe Mkuu wa Mkoa, ninawatumia
salamu za rambirambi na pole nyingi familia, ndugu, jamaa na
marafiki waliopotelewa na wapendwa wao
kwenye ajali hiyo. Ninamuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema azilaze mahali pema peponi roho
za Marehemu wote, Amina”, ameongeza
kusema Rais Kikwete.
Hata hivyo Rais Kikwete
amesema, pamoja na majonzi
makubwa waliyo nayo wafiwa, anawaomba
wawe wavumilivu, watulivu na wenye
moyo wa ujasiri
katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya wapendwa
wao, na kwamba
yeye binafsi yuko pamoja nao
katika msiba huo.
Kwa upande wa watu
waliojeruhiwa katika ajali hiyo, Rais
Kikwete anawaombea kwa Mwenyezi Mungu
ili waweze kupona haraka na
kuungana tena na ndugu na
jamaa zao, hivyo kuendelea na maisha kama
ilivyokuwa awali kabla ya kutokea
kwa ajali.
Rais Kikwete amesema kwa vile ajali
za barabarani zinaoneakana kukithiri katika siku za
karibuni, amezitaka mamlaka zote zinazohusika
na usimamizi wa Sheria ya
Usalama Barabarani kubuni mbinu zitakazowezesha
kudhibitiwa kikamilifu kwa ajali za
barabarani ambazo zinasababisha kupotea kwa maisha ya
watu wengi wasiokuwa na hatia,
hivyo kulinyang’anya Taifa rasilimali muhimu isiyokuwa na mbadala kwa
maendeleo ya nchi yetu.
Amesema hivi sasa angependa
kuona hatua kali zikichukuliwa dhidi ya madereva wanaosababisha
ajali hizo kwani nyingi zinaonekana
kusababishwa na
ukosefu wa umakini wa madereva
wanaoendesha magari kwa mwendo wa
kasi na hatimaye
kushindwa kuyamudu inapotokea dharura yoyote barabarani.
Aidha, Rais Kikwete amesema
ni wakati
sasa wa kuangalia
kama madereva wanapata mafunzo yanayostahili kwa kazi
“Nina
hakika kwamba mambo yote hayo yakifanyika
inavyopasa, Taifa letu litaondokana na jinamizi hili
la ajali za barabarani na hivyo
kuepuka vifo vya watu wengi
vinavyotokea bila sababu za msingi”,
amemalizia Rais Kikwete kwenye salamu zake za
rambirambi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
10 Agosti, 2010