DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Mheshimiwa Henry Shekifu kutokana na ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jana
tarehe 6 Agosti, 2009 katika kijiji na Kata ya Gehandu wilayani Hanang, Mkoani
humo ambayo imesababisha vifo vya watu 10 na wengine 36 kujeruhiwa.
Ajali
hiyo ilitokea wakati basi la Kampuni ya
“Ni
kwa masikitiko na majonzi makuu ninakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Mheshimiwa Henry Shekifu salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 10 vilivyosababishwa na
ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jana tarehe 6 Agosti, 2009. Kupitia kwako, natoa pia pole nyingi kwa watu
wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo huku nikiwaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone
haraka na wapate nafasi ya kuendelea na shughuli zao za kawaida”, amesema Rais
Kikwete katika salamu zake.
Katika
salamu hizo, Rais Kikwete, hali kadhalika, amewatakia moyo wa uvumilivu na
subira ndugu, jamaa na marafiki wa wote waliofariki katika ajali hiyo katika
kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya wapendwa wao.
Aidha
katika salamu hizo za rambirambi, Rais Kikwete amerudia kukemea tabia ya ukiukwaji
wa sheria ya usalama barabarani na hivyo kusababisha upotevu wa maisha ya
watu na uharibifu wa
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
08 Agosti, 2009