UNITED
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE
HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
WA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Ajali hiyo ilihusisha magari mawili,
moja likiwa basi dogo aina ya Toyota Hiace mali ya Kampuni ya Sayona Trans lililogongana
uso kwa uso na lori la mafuta lenye tela aina ya Scania na hatimaye kuwaka moto
uliochangia sana kuteketeza maisha ya abiria hao 10 waliokuwemo kwenye basi
hilo na kuwajeruhi wengine.
“Kwa dhati ya moyo wangu, nachukua
fursa hii kukutumia salamu za rambirambi wewe Mkuu wa Mkoa kutokana na ajali
hiyo iliyosababisha kupotea kwa roho za watu 10 wasiokuwa na hatia yoyote”,
amesema Rais Kikwete katika salamu zake, na kuongeza, “kupitia kwako, natuma
salamu za rambirambi na pole nyingi kwa familia zilizopotelewa na wapendwa wao
kutokana na ajali hiyo, huku nikimuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema
aziweke mahali pema peponi roho zao, Amina”.
Katika salamu hizo, pia Rais Kikwete
amesema anawaomba wote waliofikwa na msiba huo mkubwa wawe na moyo wa uvumilivu
na ujasiri wakati wote wa maombolezo.
Amesema anamuomba Mola awajalie wapone haraka wote waliojeruhiwa katika
ajali hiyo na awawezeshe kuungana tena na ndugu, jamaa na marafiki zao ili
waendelee na maisha
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27
Julai, 2010