UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia salamu za rambirambi
Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Omar Nundu kufuatia kifo cha ghafla cha Sylvester Rwegasira, aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Chama Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kilichotokea
tarehe 4 Aprili, 2011 kutokana na maradhi
ya moyo.
Rais Kikwete amesema kuwa kifo cha Sylvester Rwegasira kimeleta simanzi kubwa siyo
kwa familia
yake tu, bali pia jumuiya
ya wafanyakazi hapa nchini kwani
Marehemu Sylvester alikuwa mtetezi mkubwa wa wafanyakazi hususan wale wa Reli ambao yeye
alikuwa Katibu Mkuu wa Chama chao,
kwani alijitoa kwa moyo wake wote
kutetea maslahi yao.
Kupitia kwa Waziri
wa Uchukuzi, Rais Kikwete ametoa
pole nyingi kwa familia ya Marehemu
Sylvester Rwegasira kwa kupotelewa na kiongozi
muhimu wa familia, hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema aiweke mahali pema peponi
roho ya Marehemu
Rwegasira.
Wakati huo huo, Rais
Kikwete amewaomba wanafamilia ya Marehemu Rwegasira kuwa watulivu, wavumilivu na
wenye subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa
wao, huku akiwahakikishia kuwa yeye binafsi yuko
pamoja nao katika muda wote
wa maombolezo ya Marehemu Sylvester Rwegasira.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
05 Aprili, 2011