DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU
ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA
MRISHO KIKWETE KUTOKANA NA KIFO CHA MBUNGE WA RUANGWA (CCM), MHESHIMIWA
SIGIFRID NG’ITU
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa
Marehemu Sigifrid Ng’itu alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 2 Novemba, 2009 katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa.
“Ni
kwa masikitiko na majonzi makuu,
ninakutumia salamu za rambirambi kutokana
na kifo cha Mbunge wa Jimbo
la Ruangwa kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM), Marehemu
Sigifrid Ng’itu……kifo hicho kwa
hakika ni pigo kubwa kwa
familia ya marehemu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wananchi wa Jimbo la Ruangwa na Taifa kwa
ujumla”, amesema Rais Kikwete katika
salamu zake.
Rais Kikwete amemuelezea
Marehemu Sigifrid Ng’itu kama
kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa
kutokana na jinsi alivyokuwa mstari wa mbele
kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo
lake la Ruangwa na jinsi alivyokuwa anawatetea ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Rais Kikwete ameitaka
familia, ndugu, jamaa na
marafiki wa Marehemu Sigifrid Ng’itu kuwa na
moyo wa uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na kumuomba
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya
Marehemu mahali pema peponi.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
05 Novemba,
2009