UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Pwani salamu
za rambirambi na masikitiko makubwa
kufuatia ajali ya basi la abiria
lijulikanalo kama Delux Coach iliyotokea jana tarehe 25.10.2011.
“Hii ni ajali mbaya
sana, ni ajali ya kusikitisha
sana na ya
kuhuzunisha kwa wananchi wote na
hasa mimi” Rais amesema na
kusisitiza kuwa ajali kama hizi
zinazidi kutoa changamoto kwa Polisi na Vyombo
vya Usalama Barabarani.
“Huu ni mtihani zaidi
kwa Polisi na Vyombo Vya
Usalama Barabarani, tunahimiza sheria za barabarani zifuatwe
na kuzingatiwa, na hili ni
pamoja na usalama wa vyombo
hivyo na abiria wake, hii ni changamoto kubwa
kwa polisi katika kulisimamia hili na kuona
linatekelezwa” Amesema.
Rais amezidi kuwakumbusha Polisi wa
Usalama Barabarani kutolegeza kamba au kuwa waangalifu tu pale ajali inapotokea
na kulegeza kamba mara baada
ya tukio kuisha.
“Hili ni eneo ambalo
litazidi kuwa tatizo siku hadi
siku kama hamtakuwa makini na kuonesha
ushupavu kwa wale wote wanaovunja sheria na kutozingatia mahitaji ya chombo salama
cha usafiri wa binadamu na mali
zao wakati wote”. Amesisitiza.
“Nawapa pole wafiwa wote, nawatakia waliojeruhiwa kupata ahueni haraka iwezekanavyo
na kurudi katika shughuli zao za kila
siku.” Rais amesema.
Kulingana na taarifa
ya awali ya Polisi, Basi
lilipasuka tairi la mbele kulia, likaachia
njia na kusababisha
kupinduka na ghafla likawaka moto na kusababisha
vifo na majeruhi.
Ajali hiyo imetokea katika
eneo kati ya Kongowe na Misugusugu kwenye barabara kuu ya Dar-Morogoro
ambapo basi hilo lilitokea Dar kuelekea Dodoma.
Taarifa inasema basi liliondoka
Dar likiwa na
abiria 42 na kufika Kibaha lilipakia
wengine watano, hivyo pamoja na
dereva na utingo basi likawa
na abiria 49 wakati wa ajali.
Hadi sasa taarifa kamili
ya waliopoteza maisha bado haijathibitishwa
kutokana na
basi kuungua na kusababisha kuungua kwa baadhi
ya abiria, ambapo mafuvu matano
yameokotwa katika eneo la ajali na
watu 8 hawafahamiki waliko.
Taarifa inaendelea kueleza kuwa abiria 36 inasemekana wamejiokoa kwa kupitia
madirishani baada ya kupata maumivu,
kati yao wanaume 27 na wanawake
9 wote wamepelekwa katika hospitali teule ya Tumbi
ambapo wanawake wawili wamelazwa na wengine wametibiwa
na kuruhusiwa.
Mwisho.
IMETOLEWA
na Premi
Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
26
Oktoba, 2011