UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Katika rambirambi
zake, leo, Jumanne, Machi 9, 2010, Rais Kikwete amesema kuwa ameshitushwa mno
na kuhuzunishwa na mauaji ya mama huyo, aliyekuwa na umri wa miaka 65, yaliyotokea
katika mazingira ambayo hajafafanuliwa.
“Nimepokea kwa
majonzi na huzuni nyingi kifo cha Mama Anna Daraja. Nilipata kumfahamu binafsi
Mama Daraja. Alikuwa mtu mwema na mpenda watu.” Amesema Rais Kikwete katika
rambirambi hizo na kuongeza:
“Napenda kwa dhati
ya moyo wangu kukutumia wewe, ndugu Andrew Daraja pamoja na familia yako yote,
ndugu na jamaa zako wote, rambirambi zangu za moyoni kabisa kutokana na kifo
hiki cha ghafla.”
Ameongeza
Mheshimiwa Rais: “Mawazo yangu na ya familia yangu, yako nanyi katika kipindi
hiki kigumu cha kuondokewa ghafla na mpendwa wenu. Namwomba Mwenyezi Mungu
awapewani nguvu na subira kuweza kuwa na uvumilivu wa kuvuka kipindi hiki. Ni
mapenzi yake Mwenyezi Mungu.”
Balozi Daraja
alistaafu utumishi wa Serikali Septemba 2007, baada ya kuwa ametumikia katika nafasi
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa Balozi wa
Pia Balozi daraja
alipata kuwa mwandishi wa hotuba, na baadaye kuwa mshauri wa masuala ya
kibalozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
09 Machi, 2010