UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JAKAYA
MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia salamu za rambirambi
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya,
Mhe. Abbas Hussein Kandoro kufuatia vifo vya
watu 14 na wengine 40 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya
barabarani iliyotokea tarehe 25 Septemba, 2011 katika kijiji cha Mbuyuni, wilayani Chunya, Mkoa wa
Mbeya baada ya gari aina
ya Mitsubish Fuso walilokuwa wakisafiria kupinduka wakitoka kweye mnada Wilayani
humo.
“Nimeshtushwa,
na kusikitishwa
kwa Taifa letu kupoteza, kwa mara nyingine,
roho za Watanzania
wenzetu 14 waliofariki kutokana na ajali
mbaya ya barabarani katika eneo la mkoa wako,”
amesema Rais Kikwete katika salamu zake na
kuongeza:
“Naomba unifikishie salamu zangu za
pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao katika
ajali hii mbaya. Nawahakikishia kwamba nipo pamoja
na familia hizo katika kipindi
chote cha maombolezo kwani msiba huu
ni wetu sote.” Rais Kikwete amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azilaze pema peponi
roho za marehemu
wote.
Aidha, amesema anawaombea kwa Mola
wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo
wapone haraka ili waweze kuungana
tena na familia
zao na kuendelea
na maisha yao ya kawaida.
Amesema kutokana na kukithiri
kwa ajali za barabarani ambazo
zimeendelea kulinyang’anya taifa nguvukazi muhimu kwa maendeleo
ya nchi yetu,
vyombo vyote vinavyohusika na usalama wa barabarani
havina budi kusimamia kwa karibu
mwenendo wa vyombo vya usafirishaji
wa abiria ili kuepusha kutokea
kwa ajali zaidi za barabarani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
27
Septemba, 2011