DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali ya Awamu ya
Nne imedhamilia
kuendeleza kwa dhati hazina ya
mradi wa Makaa ya Mawe
ya Mchuchuma na yale ya
Liganga kwa ajili ya kuendeleza
na kuleta maendeleo kwa wananchi. Rais Jakaya Mrisho Kikwete
amewaambia wananchi wa Ludewa
katika mkutano wa hadhara uliofanyika
leo katika uwanja wa mpira
sabasaba.
“Dhamira yetu ni kuyaendeleza madini haya na
baada ya muda mfupi tutatoa
taarifa ya maamuzi yetu ya
jinsi ya kuendeleza madini haya”. Rais amesema
Rais amesema kuendelezwa kwa Linganga
na Mchuchuma ni moja ya
ahadi za Ilani ya Uchaguzi
ya Chama cha Mapinduzi iliyoitoa wakati wa uchaguzi mwaka
2005.
Rais Kikwete amewaeleza wananchi kwamba kazi ya utafiti
katika makaa ya mawe ya
Mchuchuma imeshakamilika hata hivyo yale ya Liganga
bado utafiti unahitajika zaidi na serikali inatafuta
namna ya kuharakisha tafiti hizo. Ili kuendeleza raslimali hizi zenye uwezo
mkubwa wa
kusukuma maendeleo katika mikoa ya
kusini.
“Tulichoamua ni
kutafuta njia ya haraka ya
kutuwezesha kufanikisha miradi hii”. Rais ameeleza
Tatizo kubwa katika mradi
wa makaa
ya mawe ya
mchuchuma ni namna gani makaa
hayo yatakapochimbwa yataweza kusafirishwa na kufikishwa kwenye
soko. Njia kubwa na inayofaa zaidi ni njia
ya reli ambayo
ni gharama kubwa sana. Lakini
Rais Kikwete amesema pamoja na gharama
hizo dhamira kubwa ya serikali
yake ni kuyaendeleza
madini hayo ili yaweze kuleta
maendeleo na baada ya muda
mfupi serikali itatoa maamuzi kamili ya miradi
hii.
Rais Kikwete yuko mkoani
Iringa katika shughuli za kikazi
za kukagua maendeleo na
kusikiliza matatizo ya wananchi. Mapema
leo asubuhi
Rais Kikwete ametembelea na kukagua maaka ya
mawe ya Mchuchuma
na kutembelea kituo cha Umeme cha Ludewa ambacho kimeaanza kutoa umeme kwa wananchi
wa mji wa
Ludewa na kuona maendeleo ya miradi hii. Kaitka kituo cha Umeme cha Ludema Rais ameona
machine iliyotolewa na kanisa Katoliki na kuwaeleza wananchi
kwamba tayari serikali imeangiza machine 2 nyingine kubwa zitakazokuwa na uwezo wa kutoa
kilowatt 600 kila moja ambazo zitafungwa na kuongeza umeme
katika mji wa Ludewa.
Rais Kikwete mchana huu anaelekea wilaya
ya Njombe. Akiwa wilayani humo ataendelea
na shughuli
za kikazi za kukagua maendeleo
na kuzungumza na wananchi.
Mwisho
Imetolewa na Premi
Kibanga
Ludewa
02
Agosti, 2008