DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali ya Awamu ya Nne inalipa uzito mkubwa suala la kilimo, na juhudi sasa
zinafanyika kuongeza kasi ya utekelezaji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema leo wakati akihutubia mkutano wa hadhara
huko Lituhi wilayani Mbinga.
Rais amesema Serikali yake imeongeza mbolea ya ruzuku toka bil.7 mwaka 2005
hadi kufika bil.118 mwaka huu.
Akizungumzia juhudi za Serikali katika kuendeleza kilimo wilayani Mbinga Rais
amesema mkoa wa Ruvuma utapatiwa matrekta ya mkono 251 na kati ya hayo 50
yatatolewa wilaya ya Mbinga na kipaumbele itakuwa kwenye SACCOS za kilimo.
“Tutatilia mkazo Kilimo cha Umwagiliaji na Matrekta na tayari mil.45 zimewekwa
katika akaunti ya wilaya yenu kwa ajili ya matayarisho ya mradi mkubwa wa
umwagiliaji.” Ameelezea.
Mapema leo asubuhi Rais amefungua Mradi wa Maji wa Jamii katika kijiji cha
Litumba Kuhamba wenye gharama ya shilingi milioni 210 uliogharamiwa kwa pamoja
na wanannchi, Serikali Kuu na Halmashauri ya Wilaya.
Rais pia amekagua kivuko cha Mto Ruhuhu na kukagua kituo cha Afya cha
Lituhi.
Rais amewapongeza wananchi wa Litumba Kuhamba kwa mradi wao wa maji na
kuwaeleza kuwa tatizo la maji ni moja ya kero kubwa alizoambiwa wakati wa
kampeni na sasa ahadi yake ya kutatua kero hiyo imetimia.
“Wilaya ya Mbinga ilikuwa na tatizo kubwa la maji tumeamua kulitatua na bado
mipango inaendelea kutafuta jawabu la kudumu, hii ni awamu ya kwanza, imeisha,
awamu wa pili inakuja”. Amesema, na kueleza kuwa nia ni kuondoa tatizo la
maji kabisa.
Mwisho.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Songea.
11 Agosti, 2009