DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ina azma ya kuwapatia wananchi wake wote maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewambia wananchi wa Mugumu, mkoani Mara leo mchana  wakati alipokuwa akiwahutubia baada ya kuzindua bwawa la Manchira na Kioski cha Maji cha Mugumu.


"Suala la maji ni moja ya vipaumbele vya Chama Cha Mapinduzi,  ifikapo mwaka 2025, kila Mtanzania apate maji safi na salama mita 400 toka alipo na utekelezaji wake unaanza sasa" Rais amesema.


Amesema Serikali imeongeza bajeti ya maji kwa sababu ya shabaha hiyo mbali na Maji vipaumbele vingine ni Elimu, Miundombinu, Afya na Kilimo.
Bwawa la Mugumu limegharimu  Serikali shilingi billioni 10.2 na ni moja ya ahadi za Chama Cha Mapinduzi kwa wananchi wa Mara ya mwaka 2005.


Mji wa Mugumu umekua na tatizo la maji kwa muda mrefu ambapo juhudi za kujenga Bwawa la Mugumu zilianza miaka 30 iliyopita wakati Rais Kikwete akiwa Waziri wa Maji.


Ahadi zingine kwa wananchi wa mugumu zilikuwa Umeme ambao tayari umepatikana, Bwawa la Mugumu ambalo leo limezinduliwa, hospitali ambayo ujenzi umeanza na barabara na kiwanja cha ndege cha kimataifa ambapo Rais amesema ahadi hii iko palepale.


Rais amesema barabara hiyo itajengwa katika maeneo ya watu na wala sio ndani ya hifadhi kama watu wengine wanavyosema.
"Kilomita 50 ndani ya hifadhi hazitawekwa lami lakin lami itawekwa nje ya hifadhi kwa wananchi ili tusiwanyime haki ya uchumi wao kuendelea".  Amefafanua


Rais pia amedokeza nia ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kujenga Chuo Kikuu kingine mkoani Mara ili kupanua fursa za Elimu Nchi.


"Kuanzia 2015-20 mtoto wa Tanzania akianza shule lazima afike Form Four na mipango hiyo ina anza sasa na ndiyo sababu elimu itaendelea kuwa kipaumbele cha mwanzo kwa muda mrefu" Rais amewaeleza wananchi na kuwataka walinde vyanzo vya maji, watunze Bwawa na kuchangia gharama kwani Bwawa limeishakabidhiwa kwao.
Mwisho.

Imetolewa na Premi Kibanga,

MUGUMU,

Mara.

02 Julai, 2010