UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania bado inaamini na kusimamia misingi na imani
ile ile iliyokuwa
nayo miaka hamsini nyuma, juu ya Umoja
wa Mataifa kama ilivyoainishwa na waasisi wa
taifa letu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
amesema hayo wakati wa kutuhutubia
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) jijini
New York Marekani, jana tarehe 22 Septemba, 2011.
“Najivunia kuwa Tanzania inaendelea kuamini misingi ya UNO, na mwanachama
hai wa baraza
hili la Dunia, tunaahidi kuendelea kuamini hivyo kwa
miaka mingine 50 na zaidi” Ameeleza .
Rais ameeleza kuwa katika
miaka hiyo 50 ya uanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania imeshiriki katika shughuli za kulinda
Amani na Usalama Barani Afrika na sehemu
nyinginezo duniani kama ilivyotakiwa kufanya hivyo na
UN.
“Siku zote tumekuwa tukiamini
kuwa mazungumzo, kuzuia na usuluhishi
wa migogoro ndiyo
njia sahihi zaidi ya ya
kutatua migogoro. Hivyo, Tanzania imekuwa siku zote
mstari wa
mbele katika kuongoza mazungumzo ya kutatua migogoro
katika nchi zinazotuzunguka, katika kanda yetu na
kwingineko Barani Afrika”. Ameeleza.
Tanzania imekuwa mstari wa mbele
katika kuchangia katika shughuli hizo kwa kutuma
polisi, jeshi na hata rai
wa Nyanja mbalimbali katika shughuli za amani za
UN na pia pamoja na Denmark mwaka 2006, zimefanikiwa kuongoza katika kuundwa kwa Kamisheni
ya Amani.
Katika hotuba yake, Rais
Kikwete amewakumbusha wajumbe jinsi Baba wa Taifa, Hayati
Julius Kambarage Nyerere alivyokataa na kupinga ukoloni na ubaguzi wa
aina yeyote ile Barani Afrika
na duniani kote na kusema
kuwa Uhuru wa nchi yetu
haungeweza kukamilika mpaka nchi zingine
zote Afrika zimekuwa huru.
Na ndipo
akaazimia kuzisaidia nchi zingine katika
harakati za ukombozi na
hatimaye uhuru wa nchi hizo.
“Kama tulivyokuwa
na amini wakati wa uhuru,
bado tunaamini leo kuwa binadamu
wote ni sawa
na wanastahili haki zote na
kulindwa na kuheshimiwa haki zao za kiraia,
kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni kama inavyoanishwa katika mkataba wa kimataifa
wa haki za
binadamu”. Rais amesisitiza na
kusisitiza kuunga mkono jitihada za watu wa
Palestina katika harakati zao za
kutafuta uhuru wao.
Amesema
Tanzania ingependa kuona nchi mbili za
Israeli na nchi huru ya
kidemokrasia ya Palestina wakiishi kwa amani na
utulivu na katika misingi ile ile Tanzania inaunga mkono jitihada
za watu wa
Cuba kutaka vikwazo vyote viondoshwe dhidi yao.
“Watu hawa katika nchi
hizi mbili wameteseka kwa muda mrefu na
umefika sasa wakati kwa mzigo
huu uondoshwe kutoka mabegani mwao”. Rais amesema.
Rais ameendelea na
mikutano na viongozi mbalimbali duniani na wawekezaji
ambao wana biashara zao nchini
Tanzania na wale wanaotaka kuwekeza Tanzania.
Mwisho.
Imetolewa na Premi
kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa RaisMsaidizi,
New
York.
Marekani.
23 Septemba, 2011