DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa
Halfa hiyo fupi itahudhuriwa na viongozi wa
taasisi zinazohusiana na masuala ya sheria, utawala bora, mapambano dhidi ya
rushwa na michakato ya uchaguzi.
Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge katika
kikao chake kilichopita mwezi uliopita inatekeleza na kuhitimisha ahadi ya Rais
Kikwete wakati wa kuzindua Bunge la sasa Desemba 30, 2005, mara baada ya
kuchaguliwa kuwa Rais wa
Rais Kikwete aliliambia Bunge wakati huo
kuwa Serikali yake ilikuwa inakusudia kuanza mchakato wa kutungwa kwa sheria ya
kihistoria ya kudhibiti matumizi ya fedha katika chaguzi nchini.
Sheria hiyo inalenga kudhibiti matumizi ya
fedha na vitendo vya rushwa katika michakato ya uchaguzi ndani ya vyama, na
wakati wa uchaguzi wenyewe baina ya vyama, kwa kuwabana watu wanaotaka kupata
uongozi kwa nguvu ya pesa.
Sheria hiyo pia itasaidia kuwabana watu
wanaogeuza haki
Aidha, sheria hiyo inalenga kuleta usawa
katika michakato ya uchaguzi baina ya wagombea mbalimbali.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
16 Machi, 2010