DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka leo mchana kuelekea Kampala Uganda kuhudhuria kikao  cha 15 cha Baraza Viongozi wa  Umoja wa Afrika (AU) kinachoanza leo 25 Julai hadi 27 mwezi huu.

Mada kuu ya mkutano huo ni Afya ya Mama na Mtoto na Maendeleo Afrika

Mbali na ajenda hiyo kikao cha viongozi kitajadili mabadiliko kuhusu kamisheni ya Umoja wa Afrika kuwa Mamlaka ya Umoja wa Afrika (Transformation of the African Union(AU) into the African Union Authority(AUA).


Pamoja na hayo kIkao kinatarajia kuteua Majaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na uteuzi wa wana kamati ya Haki za Mtoto na kujadili ripoti ya Baraza la Amani na Usalama kuhusu Afrika.

Mada inayohusu Afya ya Mama na Mtoto ni muhimu Barani Afrika na inategemewa kwamba itatoa nafasi kwa wakuu wa nchi hizi kudhibitisha msimamo wao wa kisiasa na pia kuboresha hali ya Afya ya Mama.   Na mtoto barani.


Kesho tarehe 26 Julai Rais Kikwete anatarajiwa kuongoza viongozi wa Afrika waliokatika ushirikiano wa kupambana na Malaria barani , African Leaders Malaria Alliance (ALMA).


Ushirikiano wa viongozi chini ya ALMA ulianzishwa mwezi Sepemba, 2009  katika kikao kilichofanyika chini ya Uenyekiti wa Rais Kikwete ambapo nchi 22 ziliafiki kuundwa kwa ushirikiano huo na mpaka leo nchi 28 zimeshajiunga.
Rais Kikwete anatarajia kurejea mara baada ya mkutano kumalizika tarehe 27 Julai, 2010.


Mwisho

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano,

Ikulu,

Dar es Salaam.

25 Julai, 2010