UNITED
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Tanzania
imetangaza leo,
Jumanne, Agosti 9, 2011, kuwa itatoa msaada
wa tani 300 za mahindi, ili
kuwasaidia kupunguza makali ya ukosefu
mkubwa wa chakula unaowakabili kiasi cha wananchi milioni 3.5 wa Jamhuri ya Somalia.
Tanzania
pia imeahidi kutoa misaada mingine
kwa nchi
hiyo kwa kadri uwezo wa
nchi unavyoruhusu katika kuisaidia Somalia kukabiliana na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi,
kijamii na kiusalama ambayo yamekuwa yanaikabili nchi hiyo mfululizo
katika miaka 20 iliyopita.
Mchango wa
Tanzania umetangazwa wakati
wa mazungumzo rasmi kati ya
Serikali ya Tanzania na ile ya
Jamhuri ya Somalia, na wakati wa
futari ambayo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
amemwandalia mgeni wake Rais wa Somalia, Mheshimiwa Sheikh Sharif Sheikh Ahmed ambayo
yuko katika ziara ya siku
mbili ya kikazi nchini.
“Tunasikitika
sana kuona
matatizo makubwa ya ukosefu mkubwa
wa chakula yanayoikabili nchi yako. Kama unavyojua Tanzania ni nchi masikini na uwezo
wetu siyo mkubwa. Lakini tuna methali hapa isemayo
kutoa ni
moyo siyo utajiri. Kwa hiyo
kwa moyo
huo wa mtu
masikini, tumeamua kutoa mchango wetu
mdogo wa tani 300 za mahindi
ambazo ni sawa na magunia
3,000 ili kusaidia ndugu zetu wa
Somalia kukabiliana na hali ya njaa
kubwa,” Rais Kikwete amemwambia Rais Sheikh Ahmed.
Ameongeza Rais
Kikwete: “Tunajua kuwa mahitaji yenu
ni makubwa zaidi kuliko hiki
kidogo tulichotoa. Lakini sasa ndiyo
kwanza tumeingia katika msimu wa
mavuno. Tutaangalia huko mbele kama tunaweza kuwachangia zaidi ndugu wetu wa
Somalia.”
“Tunazungumza pia na marafiki
zetu ili tuwashawishi kuona kama nao wanaweza
kuunga mkono jitihada za Serikali
ya Jamhuri ya Somalia ya kuhakikisha
inapata chakula cha kutosha ili kuokoa
maisha ya mamilioni ya wananchi.”
Wakati wa futari ambayo Rais Kikwete
amemwandalia Rais huyo wa Somalia katika Mwezi Mtukufu
huu wa Ramadhani,
Rais Kikwete ametoa mwito kwa
makampuni yanayotengeza maji nchini kusaidia
kuchangia upatikanaji wa maji kwa
wananchi hao wa Somalia. Somalia inahitaji mamilioni ya lita
za maji ili kukabiliana na ukosefu mkubwa
wa chakula na maji.
“Tutazungumza na
makampuni yanayotengeneza maji hapa nchini
kama nayo yanaweza kuchangia kupambana na janga
hili kubwa linalowakabili wananchi wa Somalia,” Rais Kikwete amemwambia Rais wa Somalia katika shughuli ya futari.
Shughuli hiyo
imehudhuriwa na
watu wengi wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Tanzania, wakuu wa mashirika
ya umma na
binafsi nchini, mawaziri, makatibu wakuu na maofisa
waandamizi wa Serikali na mawaziri
wakuu wa zamani, Mzee Salim
Ahmed Salim na Mzee Joseph Warioba.
Katika mazungumzo
hayo rasmi, Tanzania na Somalia, zimezungumza
masuala mengi ambako nchi hizo
zinaweza kushirikiana kuisaidia Somalia baada ya ujumbe wa
nchi hiyo kuelezea maeneo ambako Tanzania inaweza kuisaidia Somalia kama katika mapambano ya pamoja dhidi
ya ugaidi katika Bahari ya
Hindi na kusaidia kufundisha wataalam wa fani mbalimbali.
Rais Kikwete
pia amempongeza Rais wa
Somalia na ujumbe wake wa mafanikio ya
kijeshi dhidi ya kikundi cha kigaidi cha El Shabaab ambacho kimefukuzwa katika maeneo mengi
ya mji mkuu
wa Mogadishu ambayo kimekuwa kinayashikilia kwa muda mrefu.
Rais pia amempongeza Rais Sheikh Sharif
Sheikh Ahmed kwa mafanikio yake mengine ya kuleta
utulivu zaidi ndani ya Serikali
yake na kuongeza
muda wa utumishi
wa Serikali na Bunge kama moja
ya njia ya
kuleta maelewano ndani ya Serikali,
na kati ya
Serikali na Bunge la nchi hiyo.
Rais Ahmed ambayo
amewasili nchini leo asubuhi,
ataondoka nchini kesho baada ya
kuwa amekutana na kuzungumza na
waandishi wa habari kwenye Hoteli
ya Kilimanjanro Hyatt
Regency mjini Dard es Salaam ambako amefikia.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
10
Agosti, 2011