UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja
wa Wizara, na Naibu Makatibu Wakuu 10 wa Wizara mbalimbali.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Naibu
Katibu Mkuu mmoja kutoka Wizara moja kwenda nyingine.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es
Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bwana
George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo wa maofisa hao waandamizi wa Serikali
unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21, mwaka huu, 2011, na wataapishwa
Jumamosi wiki hii, Aprili 30, saa sita mchana.
Taarifa hiyo inasema kuwa katika
uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa, Bwana Job D. Masima kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amemhamisha Injinia Mbogo Futakamba aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Maji kwenda Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Taarifa
hiyo inasema kuwa Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni kama
ifuatavyo:
·
Bwana
Aphayo Kidata ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi wake,
Bwana Kidata alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
·
Bwana
Hab Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri.
·
Bwana
Charles Amos Pallangyo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Pallangyo alikuwa Mkurugenzi wa Uratibu – Ofisi ya
Waziri Mkuu.
·
Bibi
Mwamini Juma Malemi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi. Kabla ya hapo alikuwa Msaidizi wa
Makamu wa Rais katika masuala ya Maendeleo ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya
Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Wananchi.
·
Injinia
Mussa Ibrahim Iyombe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ulinzi
na JKT. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Usafiri katika
Wizara ya Ujenzi.
·
Injinia
Dkt. John Stanslaus Ndunguru ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Ujenzi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi katika wizara
hiyo hiyo ya Ujenzi.
·
Bwana
John Thomas James Mngodo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Uchukuzi. Kabla ya uteuzi wake alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula.
·
Bibi
Anna T. Maembe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Kabla ya uteuzi wake, Bibi Maembe alikuwa Mkurugenzi
wa Mazingira na Habari wa NEMC.
·
Bibi
Sihaba Nkinga ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi wa Sera na
Mipango katika Wizara ya Uchukuzi.
·
Injinia
Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati na Mafuta ya
Petroli.
Mwisho.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
27
Aprili, 2011