UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Clement Senzota Mwete
Mshana kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es
Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana
George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo unaanzia Alhamisi iliyopita, Aprili 21,
mwaka huu, 2011.
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Clement
Senzota Mwete Mshana alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Bwana Mshana anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Bwana Dunstun Tido Mhando ambaye amemaliza muda wake wa
utumishi kwa mujibu wa mkataba wake.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
27
Aprili, 2011