PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT OF THE

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

 

 

 

                                                      

                                                                                                                      The State House,

Tel: 255-22-2116539/2116913                                                                 P.O. Box 9120,

Fax. No. 255-22 2113425                                                                          DAR ES SALAAM.

 E-mail:  press@ikulu.go.tz                                                                       TANZANIA.

              ikulupress@yahoo.com

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

Premi Kibanga,

Bariadi,

27. Aug, 07.

 

 

Mbunge wa Bariadi Mashariki Mhe. John Cheyo amempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutimiza ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa jimbo lake wakati wa kampeni za mwaka 2005.

 

Wewe ni Rais unayetimiza ahadi zako,ulituahidi kujenga daraja mto Simiyu nakushukuru kwa hilo fedha zimekuja na mhandisi ameanza kazi, ulituahidi kutusaidia swala la bei ya pamba, kwa mara ya kwanza mwaka huu bei imekuwa nzuri sana na wananchi wameongeza juhudi katika kulima pamba, tunaomba utusaidie isishuke tena, Mheshimiwa Urais wako una baraka sana, nakushukuru kwa hiloamesema Mheshimiwa Cheyo.

 

Rais Kikwete amefika Bariadi leo na kuanza shughuli zake za kukagua miradi ya maendeleo  na utekelezaji wa ahadi zake za uchaguzi kwa kuzindua  bwawa la maji la Mwalushu lililobomoka kufuatia mvua nyingi zi.lizonyesha mwaka 2000.

 

Bwawa hilo limekarabatiwa na World Vision na Serikali inafanya mpango wa kurekebisha mfumo wa mabomba ili kusogeza huduma hiyo ya maji karibu zaidi na wananchi.

 

Akijibu shukrani hizo za Mheshimiwa Cheyo, Rais ameahidi kushirikiana na wananchi hao katika shughuli za maendeleo bila ubaguzi.

 

Tunao wajibu kuwatumikia wananchi hata kama mmemchagua mbunge wa UDP, uamuzi wenu ni wa kidemokrasia iliyokomaa ,nasi  tutaendelea kutimiza ahadi zetu kwenu, tutachimba mabwawa mengine mawili na kuhakikisha ahadi zetu kwenu zinatimia kwa kushirikiana nanyiamesema Rais.

 

Rais amewahimiza wananchi wa Bariadi kufuata kanuni kuu za ulimaji wa Pamba ili kufikia lengo la taifa la kupata kilo elfu moja kwa eka kutoka kilo mia tatu za sasa.

 

Kilio chenu kingine kilikuwa pamba, jitihada zinafanyika kuhakikisha bei haishuki bali inaimarika zaidi, nanyi zingatieni kanuni’. Amesema Rais.

 

Rais ameingia wilayani Bariadi kukamilisha ziara ya mkoa wa Shinyanga kabla ya kufanya majumuisho.

 

Mwisho.