DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa Anne Kilango
(MB), Jimbo la Same Mashariki
YAH: KUTUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA WAZIRI
WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI KWA WANAWAKE JASIRI (SECRETARY OF STATE’S GLOBAL
AWARD FOR WOMEN OF COURAGE)
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania amepokea kwa furaha kubwa
habari za kutunukiwa kwako Tuzo ya Mwanamke
Jasiri kwa Mwaka 2009 inayotolewa na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani. Aidha
anakupongeza kwa
mafanikio hayo makubwa na ya
kujivunia.
Kutunukiwa kwako Tuzo hiyo ni ishara ya kutambuliwa na kuthaminiwa kwa mchango wako
katika mapambano dhidi ya rushwa.
Aidha, ukiwa Mbunge wa
Chama Cha Mapinduzi,
Tuzo hii ni tunda la wazi
la utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya Chama Cha Mapinduzi ya 2005 kuhusu vita dhidi ya rushwa
ambayo Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake
vimetoa fursa pana zaidi kwa
wananchi, wanahabari na viongozi wakiwemo
Waheshimiwa Wabunge kushiriki kwa ukamilifu
zaidi.
Hongera sana.
Ikulu
Dar es Salaam
27 March, 2009