DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, amesema Marehemu Levy Mwanawasa wa Zambia ameishi na kuwatumikia wananchi wa Zambia kwa mapenzi, kujitolea, heshima na kwa dhati kubwa na wananchi wa Zambia wanaweza kumlipa hilo kwa kumuenzi katika matendo yake haya.

 

Rais Kikwete amewaambia waombolezaji katika viwanja vya bunge mjini Lusaka leo wakati wa Misa ya kumuombea Marehemu iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimataifa, viongozi wa dini na wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini.

 

Ameishi maisha yake na kuwatumikia watu wake kwa mapenzi, heshima na kwa ustaarabu, kitu mnachoweza kumrudishia ni kumuenzi, fuateni na tekelezeni yale aliyobakiza”.

           

Rais Kikwete ametoa salamu hizo kwa niaba ya viongozi wa  Afrika watu wake na  Tanzania ambapo amewaambia wananchi wa Zambia kuwa Mrehemu Mwanawasa alikuwa rafiki na mwenzake  kama alivyokuwa kwa viongozi wengine katika ukanda huu na duniani kwa ujumla.

 

Yeye na mimi tulipatana sana kama ilivyo kawaida kwa viongozi wa nchi mbili rafiki na majirani, siku zote tulikuwa tunawasiliana na kila mara kulipotokea jambo linalotuhusu sote tulishauriana na kwa kweli utamaduni huu ulikwenda vizuri kwa faida ya nchi zetu mbiliamesema na kumuelezea kuwa alikuwa kiongozi wa kutumainiwa na rafiki mkubwa kwa Watanzania, nchi jirani Afrika na dunia kwa ujumla na kwamba Tanzania na bara la Afrika limepoteza mtu muhimu”.

 

Rais Kikwete amesema viongozi na waombolezaji wamekuja kutoka karibu na mbali na Zambia kuja kuwafariji wa Zambia na kumshukuru Mungu kwa maisha na aliyomjalia Mwanawasa.

 

 

Premi Kibanga,

Lusaka, Zambia

 

03 September, 2008