UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS
wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameagiza chakula cha akiba cha taifa kuingizwa katika masoko ya mijini,
na hasa jiji
la Dar es Salaam, mara moja ili kupunguza
bei ya chakula
katika masoko ya miji na
kupunguza makali na gharama ya
maisha kwa wananchi.
Aidha, Rais Kikwete ameagiza
kuwa kazi hiyo ya kuingilia
soko na
kupunguza bei ya chakula kwa
wananchi iwe kazi ya nyongeza
na ya kudumu
ya Wizara ya Kilimo, Chakula
na Ushirika pamoja na Wakala
wa Akiba ya Chakula ya
Taifa (NFRA).
Amesema kuwa miji ya
Tanzania ina masikini wengi na kuwa gharama
kubwa ya masikini hao ni
bei kubwa ya chakula na
kuwa ni wajibu
wa Serikali kuchukua hatua za makusudi kuwapunguzia
wananchi gharama hizo za maisha
kwa kuingia chakula cha bei nafuu katika masoko
ya mijini.
Rais Kikwete ametoa maagizo hayo jana, Jumatatu, Machi 28, 2011 wakati alipotembelea maghala ya NFRA mjini Dar es salaam kama mwendelezo wa ziara
zake na Wizara
mbalimbali za Serikali na taasisi
za wizara hizo.
Rais Kikwete amesema kuwa kama
hatua za kuingilia soko zingechukuliwa tokea Oktoba mwaka jana
wakati bei ya mahindi ilipokuwa
sh 300 kwa kilo mjini Dar es Salaam, bei hiyo isingepanda
na kufikia sh 430 kwa bei
ya sasa.
“Hii ndiyo kazi
yetu kuanzia sasa yaani kuhakikisha
kuwa tunaingilia soko, kuingiza chakula cha kutosha na hasa mahindi kwa sababu
hiki ndicho chakula kikuu cha Watanzania na kuhakikisha
kuwa tunaishusha bei hiyo ya
mahindi hadi sh 300 katika kipindi
kifupi iwezekanavyo,” Rais amewaambia maofisa wa Wizara
na Wakala huo.
Amesema kuwa lazima viongozi
waelewe kuwa hata mijini kuna
upungufu wa
chakula. “Tafsiri ya njaa ni kama mji
haupati chakula cha kutosha basi kuna
njaa. Hivyo tujipe mamlaka ya kuingiza haraka
soko ili
kuwalinda wananchi kwa sababu hatuwezi
kuwaacha wananchi mikononi mwa wafanyabiashara
binafsi wa chakula ambacho kichocheo chao kikubwa ni faida,”
amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Hii sasa ni kazi yetu
ya kila siku
yaani kufuatilia masoko na kuhakikisha
kuwa kinakuwepo chakula cha kutosha kupunguza bei. Chezeni na
soko la Dar es Salaam ili kuhakikisha kuwa bei zinakwenda
chini haraka iwezekanavyo. Twendeni katika masoko yote
Tandale, Tandika na kwingineko
siyo kujua bei ya chakula
lakini kujua ni kiasi gani
cha chakula kinahitajika kushusha bei kwa
ajili ya wananchi.”
Amesema kuwa siyo busara
kwa mahindi
kubakia maghalani kusubiri njaa wakati
bei za vyakula
zinapanda sana. Nyie mna wajibu
wa kulilisha
taifa hili. Tuhakikishe tunaifanya kazi hii vizuri. Kazi ya kuwalisha Watanzania
haiwezi kuachiwa wafanyabiashara binafsi.
Ni kweli Serikali haitaingia katika bisahara ya chakula
lakini tunao wajibu wa
kupunguza bei na makali ya
maisha kwa wananchi.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
29 Machi, 2011