UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Shabani R. Gurumo kuwa Mnikulu
(State House Comptroller).
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Machi 9, 2011 na Katibu Mkuu
Kiongozi, Ndugu Phillemon Luhanjo inasema kuwa uteuzi
huo unaanza mara moja.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Gurumo alikuwa Naibu Katibu wa Rais.
Bwana Gurumo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu
Rajab Kianda ambaye alifariki dunia Februari 7, mwaka jana, 2010.
Mnikulu ndiye msimamizi mkuu na kiongozi wa shughuli
zote za nyumbani
za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na familia yake,
na pia ndiye
mkuu wa watumishi
wote wanaohusika na shuguli hizo.
Aidha, Mnikulu ndiye msimamizi wa Ikulu na
Ikulu Ndogo zote nchini na
ndiye hukaribisha mabalozi wapya wanaoziwakilisha nchi zao katika Tanzania wanapokwenda Ikulu kukabidhi Hati za Utambilisho wao kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
09
Machi, 2011