UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Septemba
2, 2011, amezindua rasmi Kamati ya Kitaifa
ya Misaada ya Kibinadamu kwa
Somalia ijulikanayo kama “Kamati ya Okoa
Maisha Somalia” katika shughuli fupi iliyofanyika
Ikulu, Dar es Salaam.
Katika shughuli hiyo, Rais Kikwete amewashukuru
wajumbe wa Kamati hiyo kwa
kukubali kuongoza operesheni ya kuchangisha
misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wananchi
kiasi cha milioni 3.5 wanaokabiliwa na njaa katika Somalia, kati yao 400,000 wakiwa mjini Mogadishu.
Inakadiriwa kuwa wastani wa
watu kati ya 50 na 100, wengi
wao wakiwa watoto na akinamama,
wanapoteza maisha yao katika nchi
hiyo kwa sababu ya balaa
hilo la njaa kila siku.
Wajumbe wa Kamati hiyo
ambao wote ni wafanyabiashara maarufu ni Bwana Reginald Mengi, Bwana Saidi Bakharesa, Bwana Gulam Dewji, Bwana Haruna Zakaria na Balozi
Saidi Shamo, ambao kwa pamoja
wameanzisha michango hiyo ya misaada
kwa wao kutangaza
michango yao binafsi mbele ya
Mheshimiwa Rais Kikwete.
Akitangaza michango yao mbele
ya Mheshimiwa Rais, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Bwana Mengi amesema kuwa yeye atachangia
kontena moja ya maji safi
ya kunywa, Bwana Bakhressa atatoa tani 50 za unga
wa ngano, Balozi Shamo atatoa
biskuti maalum za kushibisha kiasi
cha tani tano, Bwana Zakaria atatoa tani 50 za mafuta
ya kupikia na tani 50 za
sabuni ya unga ya kufulia
na Bwana Dewji atatoa tani 50 za unga wa
mahindi.
Bw. Mengi amemwambia Mheshimiwa Rais Kikwete kuwa misaada
hiyo ya wafanyabisahara
hao watano itaweza kujaza makontena 11 ya futi 20 kila moja
ambayo yako tayari kusafirishwa wakati wowote kuanzia
sasa kupelekwa Somalia.
Chimbuko la Kamati hiyo ni
mwito wa Mheshimiwa Rais Kikwete alioutoa wakati alipomwandalia futari ya Mwezi
Mtukufu wa Ramadhan Rais wa
Somalia, Mheshimiwa Sheikh Ahmed Sheikh Shariff wakati alipotembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi
ya siku moja
mwezi uliopita.
Mheshimiwa Sheikh Shariff ambaye alikuwa nchini kumweleza Rais Kikwete kuhusu hali ilivyo katika
Somalia na balaa ya kibinadamu linaloikabili
nchi hiyo, pia aliomba msaada
kutoka kwa Tanzania na wananchi wa
Tanzania katika kukabiliana
na balaa hilo.
Wakati wa ziara hiyo,
Mheshimiwa Rais Kikwete alitangaza msaada wa tani
300 za mahindi zenye thamani ya
kiasi cha dola za Marekani 200,000 kwa wananchi hao
na Somalia na pia alitoa mwito
kwa Watanzania wenye uwezo, na
hasa wafanyabiashara, kujitokeza kutoa michango na misaada
ya kibinadamu ili kusaidia ndugu
zetu wa Somalia.
Akizungumza na wafanyabiashara hao, Rais Kikwete
amewaambia: “Mmetupa heshima kubwa
Kwa hatua hiyo,
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.
02 Septemba,
2011