DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
RASMI YA SERIKALI KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI
imeamua kuwa kuanzia sasa walimu
nchini, kama ilivyo kwa madaktari,
wataajiriwa na kupangiwa moja kwa moja
vituo vya kazi bila kufanya
usaili ama kucheleweshwa na michakato na taratibu
nyingine za kirasimu, ili mradi
wawe wameshinda mitihani yao.
Ili
kutekeleza uamuzi huo wa Serikali, imeamuliwa kuwa walimu watapangiwa
vituo vya kazi katika miezi
ya mwisho ya mafunzo yao
ili kuwawesha kuripoti moja kwa
moja kwenye vituo vyao baada
ya kumaliza masomo na mafunzo
yao.
Uamuzi huo wa Serikali ulifikiwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika wiki iliyopita, Alhamisi, Februari 3, 2011, mjini Dar es Salaam chini ya uenyekiti
wa Rais Jakaya
Mrisho Kikwete.
Baraza limefikia uamuzi huo kwa kutilia maanani uhaba wa walimu,
kama walivyo madaktari nchini na, kwa nia
ya kupanua na kuboresha kiwango
cha huduma elimu.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU WA BARAZA LA
MAWAZIRI
07
FEBRUARI, 2011