DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema ana matumaini kuwa
Watanzania wengi zaidi watajitokeza kupiga kura katika
uchaguzi mkuu ujao tofauti na
uchaguzi mkuu uliopita, uliofanyika kote nchini tarehe 31, Octoba, 2010.
“Natumaini hali itakuwa tofauti kwa uchaguzi mkuu
ujao ikizingatiwa kuwa pia kutakuwa
na wagombea wapya, ” Rais amesema.
Rais
Kikwete amesema hayo leo
mchana mara baada ya kupokea
taarifa ya uchaguzi iliyotolewa na Jumuiya ya
Ulaya, iliyokabidhiwa kwake na Mwangalizi
Mkuu wa Taasisi
ya Uchaguzi ya Umoja wa
Nchi za Ulaya,
Bw. David Martin, katika Ikulu ya Dar-es-salaam.
Taarifa
hiyo inasema kwa ujumla,
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 31, 2010 ulikua shwari na uliendeshwa
kwa utaratibu mzuri.
Taarifa
hiyo imeelezea kuwa idadi hiyo
ndogo kwa
Tanzania Bara inaweza kufafanuliwa
kwa kutumia mchanganyiko wa sababu ambazo zifuatazo:
1.
Hali ya watu
kutojali pamoja na kuwa na imani kubwa
kuwa CCM ingeshinda kwa vyovyote vile bila kujali ni
idadi au ni kiasi gani cha wapiga kura ingejitokeza.
2. Upinzani kukosa uwezo wa
kuwaridhisha wapiga kura,
3.
Ukosefu wa
shauku ya kupiga kura miongoni
mwa watu katika nchi ambayo
imekuwa ikitawaliwa na Chama kimoja cha Siasa.
4. Kipindi kirefu cha Kampeni ambacho kilitawaliwa mno na chama
tawala.
5. Ukosefu wa
elimu ya mpiga kura.
Kwa
Upande wa
Tanzania Visiwani, taarifa inasema wananchi wa visiwani walidumisha
jadi yao ya kuwa na
ushiriki mkubwa wa wapiga kura
katika visiwa vya Pemba na Unguja.
Rais
amesema anazijua changamoto na
matatizo mbalimbali ambayo yanafanyiwa tathmini ya kutosha
ili kurekebisha hali hiyo.
Rais
pia amesisitiza kuwa ni vyema
chaguzi za nchi zikaendeshwa kutokana na taratibu
zilizopo kama zinavyoainishwa na Tume za Uchaguzi,
na pia taratibu hizo zikazingatia
mahitaji na matakwa ya nchi
na wananchi wake wenyewe.
Imetolewa
na Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari
wa Rais Msaidizi,
Ikulu
Dar
es Salaam.
07
Februari, 2011