Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
 
 
Mwanzo Profiles Cheo

Hon. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

Utumishi:
2005 - 2015 (Rais wa Tanzania)

Taarifa za Kina
Tarehe ya Kuzaliwa: 1950-10-07
Mahali pa Kuzaliwa: Msoga, Pwani

Ndoa: AmeoaMaelezo


Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alishika rasmi wadhifa wa urais mwaka  2005 na kuchaguliwa tena 2010 kwa muhula mwingine wa  miaka mitano. Rais Kikwete alizaliwa kijiji cha Msoga, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 7 Oktoba, 1950 na alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971).

Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi, na mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho. Mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na  wilaya za Nachingwea na Masasi. Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini.

Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa  Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

 
Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page